June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

WHO waipiga tafu Tanzania kukabili kipindupindu

Spread the love

SHIRIKA la Afya Duniani imetoa wa msaada wa madawa ya kuzuia ugonjwa wa kipindupindu kwa Wizara ya Afya wenye thamani ya Tsh. 42 milioni. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Msaada huo ni pamoja na vidonge vya kuulia vijidudu katika maji, katoni 1,000 na dawa ya kusafishia vyoo, lita 100, kwa ajili ya kusaidia kujikinga na maambukizi ya kipindupindu kwenye vituo mbalimbali vya hospitali.

Vidonge hivyo na maji ya kuzuia kipindupindu vimegharimu Tsh. 42,260,000, utakaowezesha mamlaka kushughulikia baadhi ya mapengo ya huduma katika vituo mbalimbali vya wagonjwa wa kipindupindu jiji la Dar es Salaam na Morogoro.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Donan Mmbando amesema msaada huo umekuja wakati muafaka huku kukiwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa ugonjwa huo, hivyo watatumia msaada huo kwa malengo husika.

Mmbando amesema idadi ya wagonjwa hadi sasa ni 380 tangu ugonjwa huo uingie nchini ambapo Dar es Salaam kuna wagonjwa 74 ambapo kambi ya Mburahati kuna wagonjwa 53, Buguruni 14 na Temeke saba.

Aidha kwa upande wa Morogoro kuna wagonjwa 60 kati yao wagonjwa 9 hadi sasa bado wapo vituoni na mmoja amefariki.

Amesema ugonjwa huo kwa sasa umeingia mkoani Pwani ambapo kuna wagonjwa saba katika wilaya ya Kibaha ambapo mgonjwa mmoja ameshafariki katika hospitali ya Tumbi.

Ameongeza kuwa ugonjwa huo unaweza kuleta athari kubwa kama wananchi wasipokuwa makini. “Ugonjwa huu tusipoudhibiti utaenea kwa kasi,” amesema Mmbando.

Kwa upande wake, Mwakilishi WHO, Rufaro Chatora amesema mambo muhimu yanayopaswa kufanyika kuzuia ugonjwa huu ni pamoja na kunywa maji safi, kufanya usafi vizuri katika vyoo.

Chatora amesema msaada huo si mkubwa sana lakini unaweza kusaidia katika maendeleo ya wagonjwa.

Pia ametoa wito kwa sekta mbalimbali kusaidiana na Wizara ya Afya katika kutatua tatizo hilo nchini ili kupunguza kasi ya kuenea kwa ugonjwa zaidi.

error: Content is protected !!