June 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

WHO kuratibu matukio ya sumu

Spread the love

ILI  kutumiza lengo la afya kwa wote, shirika la afya ulimwenguni (WHO) limeanzisha mpango wa kujenga vituo vya kuratibu matukio ya sumu katika sehemu ambazo  zina  uwezo wa kuchunguza na kutambua sumu kwa lengo la kuijengea  jamii  uwezo wa kuwa salama. Anaandika Eunice Laurian … (endelea)

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam mratibu mkuu wa kituo kipya cha kuratibu matukio ya sumu nchini, Dk Yohana Goshashy amesema mpango huo ulipelekea uanzishwaji wa vituo vingine vya kuratibu matukio ya sumu Afrika  ,serikali kupitia wizara ya  afya  na  ustawi  wa jamii  wakati huo ilipendekeza  kituo  kianzishwe  katika  maabara  ya  mkemia mkuu  wa  serikali.

Amesema sababu ya kuwepo kwa kituo cha kuratibu matukio ya sumu katika maabara ya mkemia mkuu wa serikali ni kutokana na madhara mengi ya sumu husababishwa na sumu zina asili ya kemikali, ni maabara  yenye  uwezo  wa kuchunguza  na kugundua  aina  mbalimbali  za  kemikali na sumu.

Ameongeza kuwa kituo  hicho  kitakuwa kinafanya  kazi ya uhuduma  ya utoaji wa taarifa  za  matukio  ya sumu,kuzuia  ajari za  kemikali  na kuratibu  matukio ya  sumu, kufanya  tafiti  mbalimbali zinanasohusu  sumu, kukusanya kumbumbuku  za  matukio ya  sumu na kutengeneza  kanzi  data na  nakutoa ushauri  na jinsi  ya  kutoa bita kwa  wagonjwa  walioathiriwa  na  matukio  ya sumu.

Serikali  kupitia  Wizara  ya  afya  na ustawi  wa jamii  wakati huu  ilipendekeza kituo  kianzishwe  katika  maabara  ya  Mkemia  Mkuu  wa serikali  maabara  hiyo iliendeleza  jitiahada  zilizochukua  miaka  kadhaa  na  hatimaye  mwaka  2014 kituo  cha  kuratibu  matukio  ya  sumu  nchini (NPCC) kilizinduliwa  na Mhe. Waziri  wa  afya  na  Ustawi  wa jamii.

error: Content is protected !!