February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

WhatsApp ilivyotumika kuvujisha mtihani

Whatsapp

Spread the love

BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA) limewasimamisha kazi maafisa elimu, maafisa taaluma, waratibu wa elimu na wakuu wa shule za msingi  wa Wilaya ya Chemba na Kondoa kwa tuhuma za kuvujisha mtihani wa kumaliza elimu ya msingi wa mwaka 2018 uliofanyika Septemba 5 hadi 6 mwaka huu. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji NECTA, Dk. Charles Msonde amedai kuwa, watuhumiwa hao kwa makusudi walifanya udanganyifu wa mtihani huo kwa kuunda kundi la siri la Whatsapp ambalo walilitumia kusambaza mtihani huo kwa lengo la kupandisha ufaulu wa shule za Halmahsuri ya Chemba .

Akieleze kuhusu tukio hilo, Dk. Msonde amedai kuwa, uongozi wa elimu Halmashauri ya Chemba kwa kushirikiana na waratibu wa elimu kata na wakuu wa shule waliufungua mtihani huo siku moja kabla ya terehe iliyopangwa kufanyika, ambapo waalimu hao walifanya kazi ya kukokotoa majibu yake kisha kusambaza kwa wakuu wa shule ambao walifikisha majibu hayo kwa watahiniwa.

“Tukio la halmashauri ya Chemba mkoani Dodoma, uongozi wa idara ya elimu  wa halmashauri hiyo ulipanga kwa makusudi kufanya udanganyifu wa mitihani hii ya kumaliza elimu ya msingi, viongozi walipanga kwa kushirikiana na waratibu wa elimu kata na wakuu wa shule, na ili kufanikisha azma hiyo, kamati ya mitihani ya mkoa wa Dodoma pamoja na uchunguzi wa NACTE ulibaini pasina shaka waliunda makundi ya whatsap yaliyowashirikisha uongozi wa elimu na waratinu wa elimu wakayafunga kwa siri ili wawe na mawasiliano miongoni mwao ya uhakika na haraka,” amesema na kuongeza.

“Mtihani ulipofika kwao siku moja kabla ya mtihani kufanyika tarehe 4 Septemba 2018  mitihani ilifunguliwa na kusambazwa katika makundi hayo, kwa minajili ya kukokotolewa na kupatiwa majawabu na kuwafikishia wakuu wa shule ili wapewe watahiniwa na kupandisha ufaulu wa halmashauri yao.Viongozi hawa walikuwa wakitoa maelekezo kwa waratibu namna ya kutekeleza waliyopanga waweze kufanikisha azma hiyo.”

Dk. Msonde aliwataja vinara wa mpango huo, akiwemo Kaimu Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Chemba, Modest Tarimo akisaidiwa kwa karibu na Afisa Taaluma wa Elimu Msingi wa halmshauri hiyo, Ally Akida pamoja na kiongozi aliyepewa jukumu la kutunza makundi ya whatsap ambaye ni Mratibu wa Elimu Kata wa Farkwa, Deo Phillip alishirikiana na baadhi ya wakuu wa shule.

error: Content is protected !!