Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko WFP wajipanga kumkwamua mkulima mdogo
Habari Mchanganyiko

WFP wajipanga kumkwamua mkulima mdogo

Mahindi yakiwa shambani
Spread the love

MWAKILISHI  wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Tanzania, Michael Dunford alisema WFP inaangalia namna ya kumtoa mkulima katika kilimo kidogo na kuwa na kilimo kikubwa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Aidha alisema kuwa kwa sasa dola za Marekani milioni 330 zimeingizwa nchini Tanzania na tangu mwaka 2010 zimenunuliwa tani 500,000 za chakula, kati ya hizo tani 200,000 zimetoka NFRA.

Dunford alitoa kauli hiyo Jijini Dodoma muda mfupi baada ya Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga kutishia kuufuta Wakala wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA), kama hautakuwa na uwezo wa kununua tani laki tano za mazao kwa wakulima.

Hasunga alitoa tishio hilo wakati alipokuwa akizindua mashine maalum ya kusafisha mahindi iliyotolewa na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwa NFRA, jijini hapa.

Waziri huyo alidai kwa sasa kuna mabadiliko makubwa yanayokuja kufanyika NFRA kwa kuwa siyo kazi yao kuhifadhi tu chakula bali lazima wanunue mazao yote kwa wakulima na wakauze.

“Nimewashangaa mpo kwa ajili ya kuhifadhi eti chakula cha Taifa, wakati mazao yapo kwa wakulima badala ya kwenda kutafuta masoko mkayanunue mazao yaliyopo kwa wakulima, kuna masoko kama nchini Misri nendeni mkatafute masoko,” alisema.

Kufuatia hali hiyo, Hasunga alitaja mambo matatu yanayotakiwa kufanyika na NFRA ili isifutwe.

Aliyataja mambo hayo na kusema kuwa ni: “Jambo la kwanza lazima muwe na uwezo wa kununua tani laki tano kama hamna uwezo nitafuta NFRA, nunua na kuuza  si kuhifadhi tu, sio mnakaa hapa hata kutafuta masoko hamtafuti,” alisema.

Aliongeza kuwa: “Hilo sikubaliani nalo, nategemea mnunue mazao kwa wananchi, mnasema hamna mtaji wakati mnao, nunua uza, nunua uza,Hapa mnajifanya mpo ‘busy’ kwa hizo tani 36,000 za WFP hapana mnatakiwa kufanya kazi zaidi.”

Hasunga alisema jambo la pili ni lazima wawe na maghala ya kuhifadhi vizuri mazao kwa miaka mitano kutokana na kwasasa yaliyopo yanaweza kuhifadhi kwa miaka miwili au mitatu tu baada ya hapo yanakuwa yameharibika.

“Mtafute maghala mazuri kama Marekani wanaweza kutunza kwa miaka 10 hadi 15 kwanini sisi? jambo la tatu lazima mbadili mfumo wa ununuaji nafaka, mfumo mnaotumia una gharama kubwa, kuna mifumo mizuri ipo ya kielektroniki,” alisema.

Hasunga alisema kama wasipopunguza gharama za uendeshaji atawaondoa huku akitolea mfano gharama za usafirishaji kwa gunia moja ni Sh.7,500 wakati watu binafsi wanasafirisha kwa Sh.3,000 hadi 2,000.

“Hilo sitakubadiliana nalo, kwa hiyo mbadilishe mfumo na fikra zenu msipobadilisha nitabadilisha kwa lazima,” alisisitiza.

Akizungumzia Mpango mkakati wa WFP wa miaka mitano, Hasunga alisema unaendana na mpango wa serikali wa kufikia maendeleo endelevu ya dunia,ikiwemo mpango wa kuwasaidia wakulima wadogo unaendana na Programu ya ASDP II.

“Serikali ya awamu ya tano inathamini na kupongeza WFP kwenye masuala ya chakula na lishe, lishe bado ipo chini tuwahimize watu kula chakushangaza wanaoumwa ni wakulima wanaozalisha,” alisema.

Aliagiza wakulima wapewe elimu ya kutosha ya kuhakikisha wanakula vizuri, kufanya kazi na siyo kula kwa wasiwasi.

Hasunga alisema kuwa mashine hiyo ina thamani ya Sh.Milioni 399.8 na itakuwa na uwezo wa kusafisha tani 100 kwa siku za mahindi.

“Nashukuru WFP kwa mashine hii lakini naomba muangalie uwezekano wa kutusaidia pia kwenye kanda zetu zingine,” alisema.

Hasunga alisema kilimo kina changamoto nyingi hivyo inahitajika kupata teknolojia ya kuboresha kilimo na kubadili kilimo kutoka kilimo cha kujikimu na kuwa kilimo cha biashara.

Awali, Kaimu Mtendaji wa NFRA Vumilia Zikankuba alisema wamekuwa wakishirikiana kwa muda mrefu WFP na mikakati wanayoifanya imesaidia serikali.

“Miongoni mwa mikakati ni kuboresha miundombinu ya kuhifadhi kwa kutumia teknolojia kwenye uhifadhi kwa kuwa kila siku teknolojia inabadilika,” alisema.

Alisema zoezi la kuuza tani 36,000 kwa WFP linaendelea hadi sasa wamechukua tani 20,400.

“Tupo tayari kuwauzia kadri watakavyohitaji na yatakuwa na ubora unaotakiwa,tunakuhakikishia Waziri hatutakuangusha katika soko lolote la kimataifa tutaendelea kuwauzia mazao yenye ubora,” alisisitiza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!