October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wezi wapora vifaa vya NIDA, wawili wanaswa

Spread the love

WATU wasiojulikana wametoweka na vifaa vya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), wilayani Arumeru, Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Watu hao wameiba kompyuta mpakato (laptop) mbili, kompyuta (Desk top) moja, stendi mbili, kamera mbili, stendi mbili, Extation mbili na keyboad moja.

Kwa mujibu wa Jerry Muro, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, vifaa hivyo vimeibwa usiku wa kuamkia leo tarehe 6 Januari 2020, katika ofisi hizo zilizopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.

Muro amesema, kinachofanywa kwenye wilaya hiyo ni hujuma, kwa kuwa, si mara ya kwanza kwa ofisi za NIDA kuvamiwa na kuporwa vitu hivyo.

“Hii si mara ya kwanza wizi wa namna hii kutokea, ule wa awali mpaka sasa upelelezi wake bado unaendelea,” amesema Muro na akiongeza “hii nihujuma inayofanywa kwenye wilaya hii.”

Kutokana na mkasa huo, watu wawili mpaka sasa wanashikiliwa wakihusishwa na wizi huo. Wanaoshikiliwa ni Asheri Lorubani ambaye ni mlinzi na Wilson Laizer, muhudumu wa ofisi hiyo.

Licha ya Muro kuagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi ili kubaini waliohusika, pia amewaomba wananchi kutoa taarifa.

error: Content is protected !!