August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Wezi’ dawa za binaadamu wafikishwa kortini

Spread the love

WATU saba wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuiba dawa za binaadamu, anaandika Faki Sosi.

Akisoma mashataka hayo Saada Mohammed, Wakili wa Serikali mbele ya Warialwande Lema, Hakimu Mkazi Kisutu amesema kuwa, washitakiwa sita kati ya saba kwa pamoja wanakabiliwa na kosa la kula njama za kuiba mali zilizokuwa zikisafirishwa.

Washitakiwa hao ni Mathias Kiumbe (60) Mkazi wa Kigogo, Kinondoni; Said Pazi (45), Mkazi wa Temeke; Sweetbert Machine (35), Mkazi wa Kimara; Flichism Mrema (40), Mkazi wa Kimara; Nesto John (21), Mkazi wa Kimara na Adam Mzava; Mkazi wa Kigamboni.

Washitakiwa hao wanatuhumiwa kutenda kosa la pili Machi 22 kwamba waliiba dawa za binaadamu aina ya Ceftriaxone za Sindano USF 1000 NG, KOCEF zenye thamani ya Sh. 180 Milioni mali ya Abas Mohammed zilizokuwa zikisafarishwa kutoka bandari ya Tanzania kwende katika bandari kavu ya AMI ICD.

Mshitakiwa namba saba Sia Swai (36), Mkazi wa Kimara anatuhumiwa kwa kukutwa na boxi 183, za dawa za binaadamu aina ya Ceftriaxone zinazodhaniwa kuwa za wizi.

Washitakiwa wote wamekana mashitaka yote, dhamana ya washitakiwa hao Sh. 10 Milioni kwa kila mmoja na wadhamini wawili imewekwa wazi. Upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika ambapo imeghairishwa mpaka Aprili 18 mwaka huu.

error: Content is protected !!