WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji amewataka wamiliki wa viwanda vya saruji na sukari kupunguza urasimu katika utoaji wa bidhaa hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Dk. Kijaji ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo tarehe 11 Aprili wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa bei za bidhaa nchini.
Amesema urasimu huo unasababisha upungufu wa bidhaa kwenye soko na kufanya bei kuongezeka pasipo sababu za msingi.
Amesema baada ya kukutana na wadau wa sekta hizo bei hizo zimeshuka ikilinganishwa na nchi zingine za Afrika Mashariki.
Amesema bei ya saruji imepungua kutoka Sh 17,000 kwa mfuko mmoja wa kilo 50 hadi Sh 16, 125 kwa bei za mwezi Machi.
Aidha, amesema bei ya sukari nayo imepungua hadi kufikia Sh 2,670 kutoka Sh 3,000.
Leave a comment