January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wenje: Miswada ya gesi inawanufaisha vigogo

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, (Chadema), Ezekiel Wenje

Spread the love

MBUNGE wa Jimbo la Nyamagana,( Chadema), Ezekiel Wenje, amesema Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imekuwa ikipitisha miswada ya madini na gesi kwa hati ya dhararu ambayo kwa kiasi kikubwa inawanufaisha vigogo. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Kauli hiyo aliitoa  wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Shule ya msingi Mbugani.

Katika mkutano huo uliokuwa na lengo la kuwaeleza Wananchi utekelezaji wa maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano,  ulihudhuliwa na Mbunge wa Muhambwe  Kigoma, Felix Mkosamali.

Wenje amesema Serikali ya CCM mwaka 1997  ilipitisha sheria ya uchimbaji wa madini kwa hati ya dharura na sasa  wamepitisha  miswada juu ya petrol, usimamizi wa mafuta na gesi na muswada juu ya tasnia ya uzinduaji Tanzania ambayo itasababisha taifa kukosa mapato.

Amesema Serikali imekuwa ikishindwa kuwathamini Wananchi na badara yake imekuwa ikisaini sheria za madini na gesi ambayo inaacha mwanya wa rushwa wakati wauingiaji wa mikataba na wawekezaji. 

Hata hivyo amesema  Serikali imeonyesha udhaifu mkubwa katika sekta nyeti na mhimu katika ukuaji wa maendeleo na kusababisha watanzania kuwa masikini kila kukicha.

“Wabunge wa upinzania mbungeni tumekuwa tukipigania haki ya wananchi lakini hawa wabunge wa CCM wao wenyewe kazi yao ni kupinga na kulazimisha upitishwaji wa mishwada kwa hati ya dharura.

“Nadhani nyie wenyewe ni mashahidi tulivyopambana siku ya kwanza wakati miswada inaletwa bungeni, tulipambana kadri ya uwezo wetu kuipinga kujadiliwa na kupitishwa lakini wanaccm walituondoa bungeni,” amesema Wenje.

Mbunge wa Muhambwe NCCR mageuzi, Felix Mkosamali, amewataka watanzania kuendelea kukiamini Chadema, kukichagua katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba.

Mkosamali amesema wabunge wa upinzania wamekuwa wakifanya kazi kubwa kuisimamia Serikali na kuishawishi kuwatatulia wananchi kero zao hivyo ni vyema wakaendelea kukuamini chama hicho.

error: Content is protected !!