January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wenje amchachafia waziri Majaliwa

Mgambo wa Jiji akifunga gari lililoegeshwa pasipostahiri

Spread the love

SERIKALI imetakiwa kueleza kama ni halali mtu kufungiwa gari lake sehemu aliyoegesha gari wakati hakuna kibao chochote kilichoonyesha kibao cha maegesho. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa leo  bungeni na Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje (Chadema) ambaye amesema  mara nyingi mtu anaegesha gari lake eneo ambalo hakuna kibao kinachoonyesha usiegeshe gari na baadaye gari hilo linafungwa na kutakiwa kulipa faini ya Sh. 30,000.

“Mimi nataka kujua ni halali kwa mtu kufungiwa gari lake sehemu ambayo hakuna kibao kinachoonyesha hapa hakuna mtu kuegesha gari.

Akijibu swali hilo, Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kassim Majaliwa  alikiri kuwa bado kuna msongamano mkubwa wa magari kwenye makao makuu ya majiji makubwa likiwemo Jiji la Mwanza. 

Amesema  wameziagiza mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha kuwa wanaweka alama kwenye  maeneo ya kuvuka, kuegesha magari na watembea kwa miguu ili kuepusha adha hiyo.

Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Mbulu, (Chadema), Mustapha Akunaay alitaka kujua kwa nini hapa Tanzania baadhi ya Majiji na Manispaa zimebinafishwa wajibu huo.

Akijibu swali hilo, Majaliwa amesema “Ni kweli kuwa suala la uegeshaji wa magari mjini limasimamiwa na sheria ya usalama barabarani Na. 30 ya mwaka 1973.”

Aidha, amesema  zipo sheria mbalimbali zinazosimamia suala la maegesho mijini.

error: Content is protected !!