August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wenger: Ramsey yupo fiti kurejea uwanjani.

Spread the love

Kocha wa klabu ya Arsenal ya nchini England Arsene Wenger amethibitisha kiungo wake raia wa Wailes Aaron Ramsey atarejea dimbani katika mchezo unaofuta wa ligi dhidi ya Sunderland baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu.

Kiungo huyo alikaa nje ya uwanja baada ya kupata majeraha ya misuli katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa ligi kuu dhidi ya Liverpool waliopoteza kwa mabao 4-3 katika uwanja wa Emirates.

Pamoja na kurejea uwanjani mwishoni  wa wiki hii, lakini kiungo huyo amekuwa akisumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara kila msimu kitu ambacho kinaweza kusababisha kiwango chake kupungua au kustaafu mchezo wa soka katika umri mdogo kama ilivyokuwa kwa kiungo Owen Hagreves.

Licha ya ulejeo wa Ramsey ndani ya kikosi hicho, Wenger aliongezea kuwa huwenda kukawa na taarifa nzuri juu ya kurejea kwa Kiungo mshambuliaji mwingine Saint Carzola ambaye  nae alikuwa anasumbuliwa na majeraha na ijumaa ya wiki atafanya vipimo vya mwisho kama ataweza kutumika katika mchezo ujao.

Arsenal mpaka sasa inashikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu nchini England baada ya kucheza michezo tisa na kupata pointi 20 wiki hii wanakwenda kucheza na Sunderland ambao mpaka sasa hawajaonja ladha ya ushindi kwa wmichezo tisa.

error: Content is protected !!