Tuesday , 21 March 2023
Habari MchanganyikoMichezo

Wema Sepetu hatua nyuma

Wema Sepetu akiwasili kituo cha Polisi cha Kati
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imepokea hati ya upekuzi wa nyumbani kwa Wema Isaac Sepetu anayekabiliwa na tuhuma za matumizi ya madawa ya kulevya, anaandika Faki Sosi.

Uamuzi huo umetangazwa mahakamani leo baada ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba kukataa pingamizi lililowekwa na mtuhumiwa kupitia wakili wake, Peter Kibatala.

Wema ambaye ni msanii maarufu wa filamu nchini, alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza tarehe 22 Februari mwaka huu pamoja na Matilda Abass na Angelina Msigwa waliotajwa kuwa ni wafanyakazi wake wa ndani, na kusomewa shitaka moja la utumiaji madawa ya kulevya aina ya bangi. Alikana shitaka.

Uamuzi wa mahakama kuhusu hati ya upekuzi wa nyumbani kwake, ulitolewa kufuatia pingamizi aliloweka akieleza kuwa utaratibu wa upekuzi haukufanywa kwa kuzingatia vigezo vya kisheria. Aliomba mahakama isipokee hati hiyo kama kielelezo katika kesi.

Upande wa Jamhuri uliwasilisha hoja kuwa hauoni sababu ya msingi kisheria ya kukataa hati hiyo kutambuliwa kuwa ni kielelezo katika kesi kwa kuwa upekuzi haukufanywa maungoni mwa mtuhumiwa na pia ulishuhudiwa na mashahidi kama sheria inavyoelekeza.

Hakimu Mkazi Mkuu Simba amekataa hoja za wakili Kibatala akisema maelezo hayakuishawishi mahakama kuiona sababu ya kukubali ombi la mweka pingamizi.

Amesema mahakama inakubaliana na hoja za jamhuri kuwa upekuzi aliofanyiwa Wema haukuhusisha maungo yake isipokuwa ulifanywa ndani ya nyumba yake.

Baada ya uamuzi huo, Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde aliieleza mahakama kuwa jamhuri italeta mashahidi wawili kutoa ushahidi mahakamani ili kuendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo. Aliomba mahakama ipange siku ya usikilizaji.

Kesi hiyo itaendelea tarehe 16 Novemba mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania yakabidhi rasmi msaada nchini Malawi

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Bashe: Tumeshagawa pikipiki 5,500 kati ya 7,000 kwa maafisa ugani

Spread the love  WAZIRI wa Kilimo, Hussen Bashe, amesema wizara hiyo tayari...

Habari Mchanganyiko

Spika Tulia awapa neno mawaziri utekelezaji mashamba ya pamoja

Spread the love  SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amewataka mawaziri kushirikiana...

Habari Mchanganyiko

Ukosefu wa maadili kwa wakunga, wauguzi bado changamoto

Spread the loveIMEELEZWA kuwa vitendo vya uvunjifu wa maadili kwa  wauguzi na...

error: Content is protected !!