March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wema Sepetu azidi kusota mahakamani

Wema Sepetu (kulia) akitoka na mama yake mahakamani Kisutu

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imehailisha usikilizwaji wa kesi  ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili msanii wa Filamu nchini Wema Sepetu mpaka Novemba 24, mwaka huu, anaandika Faki Sosi.

Kesi hiyo ipo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba ambapo leo upande wa Jamhuri ulidai kuwa utafika mahakamani hapo na mashahidi wawili.

Wema  alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Februari 22, mwaka huu pamoja na Matilda Abass na Angelina Msigwa waliotajwa kuwa ni wafanyakazi wake wa ndani na kusomewa shitaka moja la utumiaji dawa ya kulevya aina ya bangi. Alikana shitaka.

Awali Oktoba 31, mwaka huu, mahakama hiyo ilitoa uamuzi wa mapingamizi yaliyowasilishwa na wakili wa utetezi Peter Kibatala wa kupinga hati ya ukamataji mali iliyowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mashtaka.

Hakimu Simba alipokea hati hiyo ya baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili na kuingiza kwenye rekodi za mahakama hiyo.

error: Content is protected !!