November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wema Sepetu afikishwa mahakamani Kisutu

Spread the love

WEMA Sepetu, Miss Tanzania mwaka 2006 na mwigizaji wa filamu Tanzania, amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Alhamisi Novemba Mosi, 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Pamoja na Wema kufikishwa mahakamani hapo saa 4 asubuhi na kupelekwa katika chumba cha mahabusu, lakini bado haijajulikana atashitakiwa kwa kosa gani.

Msanii huyo alitinga mahakamani hapo akiwa ameambatana na polisi kike, akiwa amevaa miwani na kujitanda ushungi kwa lengo la kujificha.

Kufikishwa mahakamani kwa Wema kunatokana na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya kukamatwa kwa msanii huyo.

error: Content is protected !!