April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wema Sepetu adakwa tena, atupwa rumande

Wema Sepetu (mwenye gauni jeusi) akitolewa mahakamani na kupelekwa mahabusu

Spread the love

WEMA Sepetu, Mwigizaji na Mshindi wa Mashindano ya Urembo mwaka 2006, amekamatwa tena leo tarehe 4 Julai 2019 na Jeshi la Magereza muda mchache baada ya mahakama kumwacha huru. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam aliamua kumwacha huru Wema kutokana na upande wa mashtaka kushindwa kupeleka ushahidi.

Hata hivyo, wakili wa Wema – Albert Msando alilalamikia hatua ya Jamhuri kushindwa kupeleka ushahidi huku ikitoa visingizio mara kwa mara.  

Hakimu Maira Kasonde amemwacha huru Wema ambapo kwa mujibu wa Kifungu cha 225 (5) cha Mwenedno wa Makosa ya Jinai, kinatoa mwanya kwa Jamhuri kumkamata tena na kumfungulia upya mashtaka.

 Gloria Mwenda, Wakili wa Serikali mbele ya hakimu leo tarehe 4 Julai 2019, aliieleza mahakama kuwa, shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini shahidi waliokuwa wakimtegemea, wamepewa taarifa kuwa anaumwa.

Kauli hiyo ilipingwa na Wakili wa Wema ambapo alidai kuwa, taarifa ya wakili wa serikali haijajitosheleza huku akihoji siku ambayo muhusika alianza kuumwa. Amedai kuwa, taarifa hiyo ilitakiwa ijitosheleze.

error: Content is protected !!