Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Michezo Wema asomewa mashtaka, aachiwa kwa dhamana
Michezo

Wema asomewa mashtaka, aachiwa kwa dhamana

Wema Sepetu
Spread the love

WEMA Sepetu, Msanii wa Filamu nchini, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shitaka la kuchapisha video yake ya ngono kupitia kurasa yake ya Instagram, mashitakiwa amekana makosa na kuachiwa kwa dhamana. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Msanii huyo ambaye pia ni Miss Tanzania namba mbili 2006, amesomewa kosa hilo na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono mbele ya Hakimu Mkazi, Maila Kasonde, amedai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja la kuchapisha video ya ngono kinyume na sheria.

Wema anadaiwa ametenda kosa hilo, Oktoba 15, 2018 katika sehemu tofauti tofauti ambapo alichapisha kupitia mtandao wake wa Instagram video yake ya picha za kingono kitu ambacho hakiruhusiwi, msanii huyo amekana kufanya kosa hilo.

Baada ya kukana wakili wa utetezi, Semwanza Rubeni alimuombea dhamana mteja wake. Hata hivyo, Wakili wa serikali Kombakono amedai kuwa licha ya dhamana ni haki ya Kikatiba anaiomba mahakama imuwekee masharti magumu kwa sababu Wema anafuatiliwa na idadi kubwa ya watu kupitia mtandao wake wa Instagram ikiwemo watoto.

Katika uamuzi wake, Hakimu Kasonde amesema anatoa masharti ya dhamana ambapo Wema anatakiwa asaini Bondi ya Sh. 10 milioni na awe na mdhamini mmoja atakayesaini kiasi hicho.

Pia amesema anatakiwa asiweke picha yoyote yenye maudhui ya ‘Ngono’ kwenye mtandao wake wa Instagram wala maneno yenye uelekeo ama viashiria vya kingono. Wema kaachiwa kwa dhamana, kesi imeahirishwa hadi Novemba 11, 2018.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Meridianbet yaibukia Tandika, yafungua duka jipya

Spread the love BAADA ya kupita maeneo mbalimbali hatimae kampuni yaMeridianbet imeibukia...

BiasharaMichezo

Ukiwa na Meridianbet ni rahisi kuwa milionea

Spread the love  CARABAO Cup raundi ya 3 Uingereza inaendelea na mechi...

Michezo

Jezi ya Samatta iliyoifunga Liverpool kuuzwa Genk

Spread the love  KLABU ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji imeamua kuanza...

BiasharaMichezo

Hii ndio historia ya El-Clasico, derby bora zaidi duniani

Spread the love  KILA nchi ina vilabu viwili hasimu na pinzani nje...

error: Content is protected !!