January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

WB: Tanzania haina ubunifu

Kero ya Maji

Spread the love

KUKOSEKANA kwa ubunifu wa kuendeleza miundo mbinu katika sekta ya elimu, maji, afya, nishati na reli na sekta nyingine kumesababisha umaskini kuendelea kuitafuna Tanzania. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Ili kuondokana na umaskini nchini, Serikali imeshauriwa kuongeza vyanzo vya mapato kutoka katika sekta mbalimbali ili kulinda uchumi wan chi.

Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Philippe Dongier, wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya ubia kati ya Tanzania na Benki ya Dunia (WB).

Maadhimisho hayo yamefanyika Jijini Dar es Salaam kuhudhuriwa na watu wapatao takribani 300 ambamo kulikuwa na Maafisa wa Serikali, Mabalozi, Wajumbe wa Sekta binafsi, na Asasi za Kiraia.

Maadhimisho hayo yalienda sambamba na uzinduzi wa chapisho la kumbukumbu ya historia pamoja na mada kuu iliyosema, “Mustakabali wa fedha za maendeleo nchini Tanzania”

Dongier amesema, licha ya kuwepo kwa historia thabiti ya kiuchumi ambayo inaonyeshwa kwa sehemu kubwa katika sekta za ujenzi, mawasiliano, na utalii, bado ukuaji wa uchumi haujaleta mabadiliko makubwa katika kupunguza umaskini.

“kunazaidi ya asilimia 40 ya watanzania wanaishi chini ya Dola za kimarekani 1.25 (shilingi 2000) kwa siku. Bado ni changamoto kubwa”

“Japo kunamatumaini ya kutokana na takwimu za hivi karibuni zinazoonyesha kupungua kwa kiwango cha umaskini kutoka asilimia 34 mwaka 2007 hadi 28 kwa mwaka 2012 lakini bado haitoshi” amesema Dongeir.

Nae Mwenyekiti wa Taasisi za sekta binafsi (TPSF) Dk. Regnald Mengi, katika mchango wake amesema, “sio kwamba Tanzania ni nchi maskini hapana ila rushwa ndio kikwazo cha maendeleo nchini.

Mengi ameendelea kusisitiza kuwa, endapo rushwa itakoma basi uchumi wan chi hautashuka kila mwananchi atapata haki yake.

“Leo tumezungumzia mambo mengi hususani masuala ya kodi na sekta ya afya ambapo tunaonekana bado tupo nyuma sana kutolana na rushwa ilioyokithiri. Pesa na misaada inatoka lakini hawafikishiwi wahusika hili ni tatizo” amesema Dk. Mengi.

Katika maadhimisho yalihudhuriwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambapo ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuisaidia Tanzania kufika hapa ilipofika kwa kusaidia katika nyanja mbalimbali hasa kilimo,miundombinu na ataendeleza ushirikiano huo.

error: Content is protected !!