July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wizara: Wasaidieni wagonjwa wa akili

Spread the love

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imetoa wito kwa kila mmoja katika jamii kuhakikisha anatoa msaada wa kutosha kwa wagonjwa wa akili ikiwa ni pamoja na kupunguza unyanyasaji na ubaguzi. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea)

Hayo yamesemwa katika tamko la wizara hiyo lililotolewa na Kaimu Katibu Mkuu, Michael John katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya afya ya akili Oktoba 10 mwaka huu, itakayoadhimishwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (WAUJ) na Chama cha wataalam wa Afya ya akili (MEHATA).

Katika taarifa hiyo John amesema kaulimbiu ya maadhimisho hayo yanayofanyika kila mwaka kwa mwaka huu ni “Utu katika Afya ya Akili” inalenga kuhamasisha jamii juu ya matatizo mbalimbali ya Afya ya Akili yanayoikabili jamii husasan kutothaminiwa kwa utu wao.

Amesema kuwa wagonjwa wa akili wanahitaji uangalizi na matunzo maalum ya kitaalam lakini pamoja na ukweli huo, huduma ya afya ya akili hazipatikani kwa urahisi katika vituo vya afya na zahanati.

Ameongeza kuwa kwa kuzingatia huduma bora zinapatikana, Serikali kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali kuhakikisha watumishi wa afya wanapewa mafunzo maalum ya namna ya kuwahudumia wagonjwa wa akili,upatikanaji wa dawa na vifaa tib, pamoja na kuboresha huduma za kizuia na kudhibiti magonjwa ya akili katika jamii.

“Hapa Tanzania wagonjwa wengi wa akili hawafikishwi katika vituo vya kutolea matibabu na badala yake kuishia kwenye tiba za jadi au kutelekezwa na kunyanyapaliwa.” Amesema John na kuongeza.

“Tanzania ina idadi ya watu 817,532 wanaougua magonjwa mbalimbali ya akili ambao pia ni ongezeko la wagonjwa 367,532 kwa kulinganisha na takwimu za mwaka 2013/14 walikua ni 450,000 ambapo mkoa wa Dar es Salaam unaongoza.”

error: Content is protected !!