MWILI wa waziri wa zamani wa Serikali ya Tanzania, Dk. Cyril Chami utazikwa Jumanne tarehe 10 Novemba 2020 kijijini kwao Kibosho, Moshi Mkoa wa Kilimanjaro. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Dk. Chami hadi mauti yamkuta usiku wa kuamkia jana Alhamisi tarehe 5 Novemba 2020 hospitalini hapo, alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).
Katika utawala wa awamu ya nne iliyoongozwa na Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete , Dk. Chami alikuwa mbunge wa Moshi Vijijini-CCM na waziri wa viwanda na biashara.
Baada ya kuingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2005, aliteuliwa kuwa naibu waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa.
Katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba 2015, Dk. Chami aliangushwa Anthony Komu wa Chadema.
Leo Ijumaa tarehe 6 Novemba 2020, Steven Chami ambaye ni msemaji wa famia, akizungumza jijini Dodoma ulipo msiba wa kaka yake Dk. Chami amesema, “tumepokea msiba kwa masikitiko na hatukuwa tunategemea ingetokea hili la kutokea.
Amesema, wataendelea na msiba nyumbani kwa Dk. Chami jijini humo hadi Jumatatu ijayo watakaposafiri kwenda Kibosho kwa mazishi yatakayofanyika Jumanne.
Dk. Chami alizaliwa tarehe 9 Februari 1964.
Leave a comment