Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri wa uchumi wa Finland atua nchini, kuteta na mawaziri 7
Habari Mchanganyiko

Waziri wa uchumi wa Finland atua nchini, kuteta na mawaziri 7

Spread the love

WAZIRI wa Masuala ya Uchumi wa Finland, Mika Tapani Lintilä amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 29 Januari hadi tarehe 1 Februari 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Lengo la ziara hiyo ni kujadili masuala ya uchumi yenye maslahi kwa Tanzania na Finland ili kuimarisha ushirikiano wa pande mbili kupitia Programu ya sasa ya Ushirikiano wa Maendeleo na biashara na kukuza ushirikiano wa kibiashara katika sekta ya biashara na uwekezaji.

Lintilă akiwa nchini anatarajia kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax; Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Pindi Chana; Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda.

Wengine ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa; Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe; Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC); Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Shirika la Umerne Tanzania (TANESCO).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

error: Content is protected !!