Tuesday , 21 March 2023
Home Kitengo Maisha Afya Waziri wa Tamisemi apewa siku 14 afike Morogoro kutatua changamoto za Afya
Afya

Waziri wa Tamisemi apewa siku 14 afike Morogoro kutatua changamoto za Afya

Spread the love

 

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo amempa siku 14 Waziri wa TAMISEMI kufika mkoani Morogoro kutatua changamoto za Afya ikiwemo za kwenye Kituo cha Afya Mikese kilichokamilika na kushindwa kutumika kwa miaka mitatu sasa ili kukifanya chama kiendelee kudumu. Anaripoti Christina Haule, Mikese … (endelea).

Chongolo alisema hayo jana akiwa Tarafa ya Mikese wilayani Morogoro wakati akifikisha siku ya 7 ya ziara yake ya siku 9 mkoani hapa kutembelea miradi ya maendeleo na kuangalia uhai wa chama ambapo alisema haiwezekani hata kidogo Serikali itoe fedha halafu miradi ikwame kwa sababu zinazotatulika.

Alisema chama hakiwezi kudumu kama mambo ya wananchi hayaendi na kwamba Serikali inampango wa kupiga hatua katika Sekta zote kimaendeleo na kuweka kuzifikia hata nchi zinazoendelea.

“Huwezi ukamwambie mwanachama kidumu Chama Cha Mapinduzi akaelewa wakati kukiwa na changamoto inasumbua ambayo ingeweza kutatuliwa kwa wakati, Waziri TAMISEMI aje arekebishe hili,” alisema Chongolo.

Hivyo aliagiza madaktari wote nane wakiwemo wa upasuaji waliopeleka kwenye kituo hicho cha Afya kujiandaa kufanya kazi kwa sababu atafuatilia na kuhakikisha kituo hicho kinaanza kufanya kazi mwishoni mwa mwezi wa Machi mwaka huu.

“Serikali imeshaleta vifaa karibu asilimia 80 bado 20 tu, sasa fedha zilizopo kwa nini msizitumie kukamilisha palipobaki na wananchi wapate huduma, sababu mnasema kituo kina miaka mitatu tangu kijengwe hakijaanza kutumika, bado ni shida kwa wananchi, tutatue hili,” alisema Chongolo.

Hata hivyo aliuhimiza uongozi kuanzia ngazi ya mkoa kuhakikisha wanasimamia na kutatua changamoto ndogo zilizojitokeza ili kukifanya kituo hicho kilichopo jirani na barabara kutoa huduma kwa wananchi hata kupokea na kuwatibu majeruhi mara ajali itapotokea kwenye barabara kuu ya Morogoro- Dar es Salaam.

Pia Chongolo alikemea tabia ya wafugaji na wakulima kuwa na migogoro isiyo na tija bali aliwataka kuwa na umoja utakaowaweka sawa katika shughuli zao za kuwaleta maendeleo.

Hivyo alimuagiza Mkuu wa wilaya hiyo, Rebecca Nsemwa kuongea na wananchi wa tarafa hiyo na wengine kwa ujumla ili kutatua changamoto hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa inaletwa na baadhi ya viongozi wanaowapa kiburi.

Awali Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Hamisi Taletale aliiomba serikali kuwasaidia kupatikana kwa vifaa tiba kwenye kituo hicho cha Afya ambavyo vinakwamisha huduma kuendelea kutolewa katika kituo hicho licha ya kukamilika miaka mitatu iliyopita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabariHabari

Ugonjwa wa ajabu wadaiwa kuua watano Kagera, Serikali yatoa tahadhari

Spread the loveJUMLA ya watu watano wanaidaiwa kufariki dunia  katika vijiji vya...

Afya

LHRC yapinga kufutwa Toto Afya: Ni ukiukaji wa sheria za watoto

Spread the love  KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimekosoa...

Afya

Manesi 7 mbaroni tuhuma za kuwauzia dawa wagonjwa usiku wa manane

Spread the love  JUMLA ya wauguzi/manesi saba wa Hospitali ya Manispaa ya...

Afya

Naibu Waziri awabebesha Wakurugenzi zigo la miradi chini ya kiwango

Spread the loveIMEELEZWA kuwa usimamizi mbovu wa miradi ya maendeleo na ujenzi...

error: Content is protected !!