ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Fred Matiang’i, anasakwa na Jeshi la Polisi nchini humo, huku sababu za hatua hiyo kutowekwa wazi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya, baadhi ya maafisa wa Polisi , jana usiku walizingira makazi ya Matiang’i kwa ajili ya kutaka kumkamata bila mafanikio.
Mtandao wa The Star kutoka nchini Kenya, umeripoti kuwa asubuhi ya leo Alhamisi, mawakili wa Matiang’i wametinga mahakamani nchini humo, kufungua madai ya mteja wao kutaka kukamatwa kinyume cha sheria akiwa nyumbani kwake na polisi wanaodaiwa kutaka kumvamia.
Kiongozi wa Umoja wa Azimio nchini Kenya, Raila Odinga, aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba, hataondoka katika makazi ya Matiang’i hadi kiongozi huyo wa zamani atakapokuwa salama.
Odinga aliyekuwa mgombea urais wa Kenya, katika uchaguzi mkuu wa taifa hilo uliopita ameandika “haramu haitalala, Kenya ni kubwa kushinda mtu yeyote mmoja. Hatutaruhusu siku za giza za ukandamizaji kurejea. Tutasimama pamoja na yeye hadi mwisho.”
Leave a comment