Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri wa Kikwete asema Tanzania hapafai kufanyia siasa
Habari za SiasaTangulizi

Waziri wa Kikwete asema Tanzania hapafai kufanyia siasa

Goodluck Ole Medeye
Spread the love

GOODLUCK ole Medeye, aliyepata kuwa naibu waziri katika serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ameibuka na kusema mazingira ya sasa nchini hayafai kufanya shughuli za kisiasa, anaandika Richard Makore.

Akizungumza na MwanaHALISI Online jijini Dar es Salaam leo Ijumaa,  Medeye amesema, “kwa hali ya  sasa ilivyo nchini, ni bora kukaa kimya.”

Naibu waziri huyo wa zamani wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi katika utawala wa Rais Kikwete amesema, “tofauti na ilivyokuwa kwenye awamu zilizopita, mazingira ya kisiasa nchini kwa sasa, siyo mazuri hata kidogo.”

Medeye ambaye aliondoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), miaka miwili iliyopita anasema, hali ya kisiasa kwa wanasiasa kufanya shughuli zao za kikatiba, siyo rafiki chini ya Rais John Pombe Magufuli.

Madeye alipata kuwa mbunge wa Arumeru Magharibi kupitia CCM. Alikihama chama hicho kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa 25 Oktoba mwaka 2015, wakati wa  “mafuriko ya Edward Lowassa.”

Aliondoka Chadema na kujiunga na chama cha United Democratic Party (UDP), kinachoongozwa na John Momose Cheyo, muda mfupi baada ya kushindwa katika kinyang’anyiro cha uspika wa Bunge la Muungano.

Medeye ambaye alidumu Chadema kwa muda usiozidi miezi 10 anasema, “mazingira ya kisiasa nchini ni magumu sana. Hivyo nimeona bora nikae nyumbani kuliko kufanya siasa.”

Hata hivyo, Madaye anamtaka Waziri wa Nishati, Merdadi Kalemani kuachia ngazi kwa kushindwa kumaliza tatizo la kukatika umeme nchini.

Amesema, “pamoja na kuamua kukaa kimya, lakini namtaka Kalemani aachie ngazi kwa kuwa ameshindwa kazi.

Amesema, “tangu juzi huku kwetu maeneo ya Bahari Beach, hakuna umeme kwa siku mbili na waziri yupo kazini. Hivyo nataka aondoke katika nafasi hiyo na kuwaachia wengine.”

Tatizo la kukatika umeme limezidi kutisa nchi na jana waziri Kalemani alitangaza kumsimamisha kazi mmoja wa maofisa wa kampuni ya umeme ya taifa (Tanesco).

Katika uamuzi wake huo, Kalemani alisema, haiwezekani nchi kuingia gizani wakati kuna watalaam ambao wanaweza kuepusha hali hiyo isitokee.

Hata hivyo, licha ya agizo hilo la waziri na kumsimamishwa kazi kwa mtumishi huyo, lakini bado mpaka sasa kuna baadhi ya maeneo hayajapata nishati ya umeme.

Medeye ni mmoja wa wanasiasa wa waliondoka Chadema na kutoa kauli za kumsifia Rais Magufuli kuwa anaendesha nchi vizuri na hivyo wanasiasa wa upinzani wamuache “anyooshe nchi.”

Alikizungumza kwa njia ya kujikomba wakati anaondoka Chadema na kujiunga na UDP, Medeye alisema, yeye ni mwanasiasa anayesimamia haki na demokrasia, na kwamba amekerwa sana na tabia ya vyama vya upinzani kutomheshimu Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson Mwansasu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa matokeo ya mtihani kidato cha nne 2022

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza matokeo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

HabariTangulizi

Bakwata wamkangaa Sheikh wa Dar es Salaam

Spread the love  BARAZA la Ulamaa, limefutilia mbali uamuzi wa “kuvunja ndoa,”...

error: Content is protected !!