January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri wa JK kuburuzwa mahakamani

Spread the love

WAZIRI wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, aweza kufikishwa mahakamani, kujibu shitaka la utapeli. Anatuhumiwa kumtampeli raia kutoka Korea, Chris Incheul Chae. Anaandika Saed Kubenea … (endelea).

Mwingine awezaye kufikishwa mahakamani pamoja na Dk. Mwakyembe, ni Victor Mwambalaswa, mbunge wa Lupa (CCM) na msemaji wa familia ya waziri huyo.

Aidha, Isaac Mwamanga, mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Dk. Mwakyembe na ambaye pia ni msemaji wa familia ya mwanasiasa huyo, naye yuko hatarini kufikishwa mahakamani katika shauri hilo.

Dk. Mwakyembe na washirika wake hao wawili, ni miongoni mwa wamiliki wa kampuni ya kuzalisha umeme kwa njia ya upepo ya Power Pool East Africa Limited.

Dk. Mwakyembe na kampuni yake, wanatuhumiwa kwa utapeli, kutokana na kukiuka makubaliano ya mkataba wa kuzalisha umeme na kampuni ya Good PM inayomilikiwa na Chris.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka Ikulu jijini Dar es Salaam, nchini Korea, watu waliokaribu na Dk. Mwakyembe na nyaraka mbalimbali, wamiliki wa kampuni hiyo wanatuhumiwa kumtapeli Chris mamilioni ya shilingi kwa njia ya udanganyifu.

Chris alitoa kiasi cha dola za Kimarekani 1.2 milioni (zaidi ya Sh. 2.6 bilioni), ili kufidia ardhi na mali mbalimbali za wananchi wa kijiji cha Kisasida, mkoani Singida. Eneo la Kisasida ndiko Dk. Mwakyembe na washirika wake wanakodai kukabidhiwa na serikali kuzalisha umeme wa upepo.

Chris anamtuhumu Dk.Mwakyembe na washirika wake kwa mambo mawili. Kwanza, fedha alizotoa hazikufikishwa kwa wananchi wa Kisasida kama ilivyokubaliwa; na pili, Power Pool East Africa Limited, imejifunga – kinyume cha taratibu –katika mkataba mwingine wa ubia na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Tayari Chris amemlima barua kampuni ya Dk. Mwakyembe, akiomba arejeshewe fedha alizotoa. Barua Chris kwenda kwa Dk. Mwakyembe imebeba Kumb. Na. PP/KOREA/22/2014. Iliandikwa tarehe 4 Februari 2014.

Katika barua hiyo, kampuni ya Korea inasema, ilijifunga katika mkataba wa ushirikiano na Power Pool East Africa, ili kuzalisha umeme wa upepo mkoani Singida.

Anasema, 22 Februari 2010, kampuni yake ilitoa kiasi cha 316, 189.60 milioni kwa ajili ya fidia ya Ardhi katika mradi huo.

Akiandika kwa wakurugenzi wenzake, mara baada ya Chris kuwalima barua, Mwamanga, anasema, “deni hilo, linayaweka mahusiano kati ya kampuni hiyo ya kigeni, katika hatari na kuchafuka mbele ya macho ya kimataifa.”

Aidha, katika makubaliano mengine, kampuni ya Chris ilikubaliana na Dk. Mwakyembe, kutoa kiasi cha dola za Kimarekani 1 milioni moja (sawa na Sh. 2 bilioni).

Nyaraka zinaoyesha, kufuatia malalamiko ya Mkorea huyo, baadhi ya wanahisa katika kampuni hiyo wenye madaraka makubwa ya kisiasa walianza kuondoa majina yao na kuomba washikiwe hisa zao na wanahisa wengine ili kuepuka kushitakiwa.

error: Content is protected !!