Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Waziri wa Fedha Kenya ajisalimisha
Kimataifa

Waziri wa Fedha Kenya ajisalimisha

Henry Rotich, Waziri wa Fedha wa Kenya
Spread the love

HENRY Rotich, Waziri wa Fedha nchini Kenya amejisalimisha kwa maafisa wa upelelezi, saa kadhaa baada ya Noordin Haji, Mkurugenzi wa Mashtaka kuagiza akamatwe. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Rotich amejisalimisha katika makao makuu ya Idara ya Upelelezi nchini Kenya leo tarehe 22 Julai 2019, kuitikia wito wa Haji.

Ni kuhusu tuhuma zinazomkabili za kukiuka muongozo wa utoaji wa kandarasi ya ujenzi wa mabwawa, wenye thamani zaidi ya Dola za Marekani 450 milioni, iliyopewa Kampuni ya Italia ya CMC de Ravenna.

Kwa mujibu wa mitandao ya Kimataifa, Rotich anahojiwa na maafisa wa upelelezi, baada ya Haji kueleza kwamba waziri huyo wa fedha pamoja na baadhi ya viongozi wengine waandamizi nchini Kenya watashtakiwa kwa kupanga udanganyifu kutokana na kushindwa kutii muongozo unaotumika katika upatikanaji wa kandarasi.

Tuhuma hizo dhidi ya Rotich ziliibuka mwanzoni mwa mwaka huu, ambapo mwezi Machi waziri huyo alikana tuhuma hizo. Vile vile, kampnuni ya Italia CMC de Ravenna ilikana kuhusika katika tuhuma hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!