Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Ummy: Corona ipo
Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy: Corona ipo

Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya
Spread the love

LICHA ya ripoti ya maambukizi ya virisi vinavyosababisha ugonjwa wa corona kupungua nchini, ugonjwa huo haujaisha nchini. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya leo tarehe 1 Juni 2020, jijini Tanga wakati wa ufunguzi wa jengo la ofisi za Makao Makuu ya Bodi ya Mkonge Tanzania.

 “Tunamshukuru Mungu hali ni nzuri, Tanga hatuna mgonjwa wa corona, kituo kilichokuwa kinatumika kwa wagonjwa wa corona kimefungwa.

“Amana tuna wagonjwa  watatu, Mloganzila  mmoja, Mwanza hakuna mgonjwa. Tunamshukuru Mungu, hata hivyo corona ipo, tuendelee kuchukua tahadhari kujikinga,” amesema Waziri Ummy.

Amesema, Tanzania imefanikiwa katika kudhibiti kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo “corona tumeishinda Tanzania, ukiangalia wenzetu, unajiuliza hivi Tanzania tuna nini? asante Mwenyezi Mungu kwa kutuokoa,” amesema Waziri Ummy.

Mara ya kwanza Tanzania iliripoti kisa chake cha kwanza cha ugonjwa wa Covid-19, tarehe 16 Machi 2020, ambapo siku moja baadae ilitangaza kufunga baadhi ya shughuli zenye mikusanyiko ya watu wengi, ili kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo.

Miongoni mwa shughuli zilizofungwa  tarehe 17 na 18 Machi 2020 ni, michezo, shule na vyuo vya kati na vikuu, pamoja na shughuli za kijamii.

Lakini Mei mwaka huu, Rais John Magufuli alitangaza kufunguliwa kwa vyuo pamoja na shughuli za michezo.

Wakati akitangaza kufunguliwa kwa shughuli hizo, Rais Magufuli alisema hatua hiyo imechukuliwa baada ya maambukizi ya Covid-19, kupungua kwa kasi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!