Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Ummy azindua mitambo ya hewa tiba ya oksijeni yenye thamani ya bilioni 1.5
Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy azindua mitambo ya hewa tiba ya oksijeni yenye thamani ya bilioni 1.5

Spread the love

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amezindua mitambo wa hewa tiba ya Oksijeni wenye thamani ya bilioni 1.5 katika hospitali ya Benjamnin Mkapa iliyoko jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Waziri Ummy amesema usimikaji wa mitambo hiyo ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha kuwa huduma zinaboreshwa na kuongeza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja mitambo 14 imeshasimikwa kwenye hospitali za rufaa za mikoa nchini.

“Sisi kama Sekta tumejiwekea vipaumbele vyetu ambavyo Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ingependa kuviona tunavitekeleza, kipaumbele kikubwa  ni ubora wa huduma za afya, hivyo mitambo hii ina lengo la kuokoa maisha kwa wananchi wake” amesema.

Waziri Ummy amesema wanatarajia kusimika mitambo mingine  57 ya hewa tiba ya Oksijeni kwenye hospitali za rufaa za mikoa,Kanda pamoja na Wilaya nchini.

Aidha, Waziri Ummy ameipongeza hospitali hiyo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Dkt.Alphonce Chandika  kwa kuhakikisha kuwa kazi ya usimikaji wa mitambo huo unakamilika kwa wakati  na unazingatia viwango vinavyotakiwa

Ameongeza kuwa mitambo hiyo haitosaidia hospitali hiyo tu bali hata hospitali na vituo vya mikoa wa Dodoma na mikoa ya jirani ikiwemo Manyara, Singid na Iringa.

Pia amesema licha ya mitambo  huo  ambao ni mradi mmoja kati ya miradi 17 ambayo inatekelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo jumla  ya takribani Bilioni 10.02 zimeelekezwa katika kukamilisha miradi hiyo hospitalini hapo.

Naye,Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt. Alphonce Chandika amesema mitambo hiyo inazalisha mitungi 400 kwa siku na una sehemu mbili ambazo hazitegemeana hivyo unaweza kuwasha sehemu moja kipindi unatumia ili kuhakikisha uzalishaji unaendelea wakati wote hata wakati wa matengenezo kinga inapolazimu kuzima upande mmoja.

Dk. Chandika aliongeza kabla ya hapo hospitali ilikua ikitumia mitungi 200 kwa mwezi  lakini kipindi cha UVIKO-19  matumizi yakiongezeka  hadi kutumia mitungi 200 kwa siku  na hivyo kuongeza gharama za uendeshaji wa hospitali na kutumia  milioni 10 kwa siku badala ya milioni 10 kwa mwezi kwa kipindi hicho cha UVIKO-19.

Bilioni 1.5 zimetumika kununua mitambo miwilli  aina ya Ozcan Kardesler Tip Cihazlari San,mitungi ipatayo 560 ya hewa tiba,gari la kusambazia mitungi ya Oksijeni pamoja na ujenzi wa jengo ambalo mitambo imefungwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!