August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Ummy aipiga ‘stop’ NHIF

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu

Spread the love

WAZIRI wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu amesitisha mara moja utaratibu mpya wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unaoweka ukomo wa mahudhurio ya mgonjwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mfumo huo ambao ulianza kutumika rasmi Agosti Mosi, 2022 pia unavitaka vituo vya kutoa huduma za afya kuwa na kibali kwanza kabla ya kutoa huduma kwa mteja wa NHIF kwa vipimo vya MRI, CT SCAN, Colonoscopy, HBA 1C, OGD, USS na ECHO.

Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Jumatano tarehe 3 Agosti, 2022 na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Catherine Sungura, Waziri Ummy ameitaka NHIF pamoja na dhamira nzuri ya kutaka kudhibiti udanganyifu, kukutana kwanza na wadau ili kuja na namna bora zaidi bila kumuathiri mteja na vituo vya huduma.

“Wizara inapenda kuwahakikishia wanachama wa NHIF na wananchi kwa ujumla kuwa itafanyia kazi mapendekezo yote yatakayotolewa na kuja na njia nzuri ili kutimiza dhamira ya Serikali ya utoaji wa huduma za afya kuanzia vituo vya afya ngazi ya msingi hadii Taifa,” ameeleza taarifa hiyo.

error: Content is protected !!