Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri Ndumbaro: Katiba iliyopo ina mapungufu
Habari za SiasaTangulizi

Waziri Ndumbaro: Katiba iliyopo ina mapungufu

Spread the love

WAZIRI wa Sheria na Katiba, Dk. Damas Ndumbaro amesema  licha ya kuwa Katiba iliyopo inafaa lakini ina mapungufu yake ndio maana Serikali imetoa muelekeo wa namna ya kufanya mabadiliko ya Katiba baada ya kupokea mapendekezo ya wananchi. Anaripoti Faki Sosi Ubwa… (endelea).

Dk. Ndumbaro ametoa kauli hiyo leo tarehe 20 Julai, 2022  jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu vipaumbele vya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Waamesema Katiba iliyopo inafaa ijapokuwa ina mapungufu ambayo yatafanyiwa marekebisho.

“Katiba iliyopo inafaa lakini ina mapungufu mimi mwenyewe kama binadamu nina mapungufu kwa hiyo ninaweza nisifae kuwa waziri labda mlete wasiri malaika.

“Katiba ya Marekani yenyewe ina mapungufu Supreme Court (Mahakama ya Juu) juzi imetoboa matundu kwenye suala la posho, umesikia Wamarekani wanasema Katiba haifai … Tuyaangalie yale mapungufu tuyajadili ili wenye mamlaka ambao ni wananchi tuyaondoe tunayondoe mapungufu hayo” amesema Dk. Ndumbaro.

Waziri Ndumbaro amesema Serikali imefungua mjadala wa kujadili katiba.

“Tuelimishane, tujue hicho tunachosema hakifai ni nini kifungu kipi na mbadala wake nini kwenye hili serikali imefungua mjadala.

“Hili si suala la wanasiasa mimi kama mwanasiasa ukiniruhusu nitasema kwanini tunafanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano, tufanye miaka kumi kwa kuwa uchaguzi ni gharama hiyo itakuwa hoja yangu lakini je, mwananchi atataka mrejesho wa huo mkataba kwa miaka kumi?  si ataona ni parefu.

“Sasa hivi hatumzuii mtu yoyote kusema Katiba hii inamapungufu tunachotaka na ndio wizara tunafungua mjadala tuambie kifungu, tueleze mapungufu, pia tueleze mapendekezo yako… utakuwa unasaidia mchakato wa kupata katiba mzuri” amesema Waziri Ndumbaro.

Waziri Ndumbaro amesema kuwa mkakati wa Serikali ni kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu Katiba na sheria.

Amesema kuwa ni muhimu wananchi waijue Katiba iliyopo, ajue upungufu na ubora wake.

2 Comments

  • Nakubaliana na waziri kabisa. Mimi kwa upande wangu ni wanasiasa
    Wenye buchu ya uongozi njoo wanashinikiza katiba ibadikishwe siyo sababu ya wanainchi ila Kwa maslahi yao wenyewe. Wanafikiri kwa kufanya hivyo, wataingia ikulu wepesi na kujinyakulia vyeo kwa ngazi tofauti. Mataifa yoote duniani, yana matatizo za katiba ila wanaheshimu katiba za mataifa yao. Kwa mataifa ya democracy zaidi ulimwenguni, katiba inabadilishwa baada ya miaka 100. Hata TZ ibadili katiba, matatizo itakuwako tuu.

  • Sherti wanainchi waelewe kuwa wanasiasa hujificha chini ya kivuli cha wanainchi. Wanapigania tumbo zao na familia zao wakitumia neno wanainchi wetu. Mfano : Tundu Lissu, ako anakula bata huko Ubelgiji inchi mbovu saana ya mabeberu, inaisumbua Congo kwa miaka mingi saana. Wanamufunza siasa za kuja kuibomowa Tanzania na watanzania wengi wasiyo juwa ukweli wanafikiri yeye ni mkombozi. Uongo mtupu ndugu zangu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!