May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Ndumbaro ataja faida za klabu ya Simba kutangaza utalii

Spread the love

 

WAZIRI wa Maliasiri na utalii Dkt Damas Ndumbalo ameimwagia sifa klabu ya Simba katika jitihada zao za kutangaza utalii na kuefunguka juu ya faida wanayopata timu hiyo ikicheza michezo ya kimataifa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Simba kwa sasa ambao ndio mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wamebakisha mchezo mmoja wa hatua ya makundi kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Akizungumza leo tarehe 23, 2022 na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati akieleze mafanikio ya Wizara hiyo katika kipind cha mwaka mmja cha uomgozi wa Rais Samia akiwa madarakani.

Waziri huyo alisema kuwa kwa sasa, Simba ni moja ya klabu kubwa barani Afrika na ndio timu inaongoza kwa kuingiza mashabiki wengi kwa mujibu wa takwimu za Shirikisho la Mpira Barani Afrika ‘CAF’ na ndio maana waliwapa jukumu la kutangaza utalii wanchi kwa kuvaa nembo ya ‘Visit Tanzania’

“Katika soka ya Afrika Simba ni kubwa sana, ukitaja timu 10 au 12 Afrika Simba haiwezi kukosa, ndio maana tuliwapa visiti Tanzania”. Alisema Ndumbaro

Kwenye msimamo wa kundi D, kwa sasa Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi saba sawa na RS Berkane waliokuwa kwenye nafasi ya pili huku nafasi ya kwanza ikishikwa na ASEC Mimosas wenye pointi tisa.

Waziri huyo aliaendelea kufunguka kuwa walitamani kuona pia klabu ya Yanga inafanya vizuri kwenye michuano hiyo, kwa kuwa nao waliwakabidhi jukumu l;a kutanza Zanzibar na Kilimanjaro lakini walitolewa kwenye raundi ya awali.

“Lakini pia hatukuwanyima Yanga licha ya kwenda mechi moja na walipigwa nyumbani na ugenini, nilitamani Yanga iendelee ili kutangaza Zanzibar na Kilimanjaro ili uonekane zaidi lakini Yanga walitolewa Asubuhi.” Alinena Waziri huyo

Yanga hapo awali ilipata nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika mwanzoni mwa msimu wa 2021/22, lakini walitolewa kwenye raundi ya awali na klabu ya Rivers united ya nchini Nigeria kwa kufungwa michezo yote miwili.

Aidha Waziri huyo aliendelea kufunguka kuwa kwa sasa Simba ndio klabu inayoingiza mashabiki wengi Uwanjani, hivyo na michezo yao kufuatiliwa na idadi kubwa ya watu kwa njia ya Televisheni.

“Simba ndio inaongoza kwa mashabiki kuingia uwanjani kwa mujibu wa takwimu za CAF, na zili mechi zote zinaoneshwa Mbashara Dunia mechi moja inaangaliwa na watu milioni 500.” Alisema Dkt Ndumbaro

Kwa sasa Simba inahitaji kushinda mchezo wake ujao wa kombe la Shirikisho dhidi ya USGN, ili iweze kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya klabu barani Afrika.

error: Content is protected !!