Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Waziri Ndalichako atoa ratiba za masomo, mitihani Tanzania
Elimu

Waziri Ndalichako atoa ratiba za masomo, mitihani Tanzania

Spread the love

PROFESA Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ametangaza ratiba ya mitihani ya kumaliza shule kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Prof. Ndalichako ametoa ratiba hiyo leo Jumatano tarehe 17 Juni 2020 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dodoma, siku moja baada ya Rais John Magufuli kutangaza shule zote zifunguliwe tarehe 29 Juni 2020.

Prof. Ndalichako amesema darasa la saba wataanza mitihani yao ya Taifa tarehe 7 hadi 8 Oktoba 2020, wakifuatiwa na kidato cha  nne ambao watafanya mitihani kuanzia Novemba 23 hadi Desemba 11 2020, kisha  darasa la nne watafanya mitihani yao tarehe 25 hadi 26 Novemba mwaka huu.

“Darasa la saba wataanza Mitihani tarehe 7 hadi 8 Oktoba, Kidato cha pili wataanza tarehe 9 hadi 20 Novemba, 9 wanaomaliza Kidato cha 4 na wa kujitegemea, wataanza Nov 23 hadi Disemba 11, na darasa la nne wataanza Novemba 25 – 26, 2020,” amesema Prof. Ndalichako.

Aidha, Prof. Ndalichako amesema wanafunzi wa kidato cha tano watapaswa kumaliza kufanya mitihani tarehe 24 Julai, 2020 na siku tatu baadaye tarehe 27 Julai 2020 wataanza masomo ya kidato cha sita.

Amesema, wanafunzi wapya wanaojiunga kidato cha tano utaratibu wao utatangazwa baadae baada ya majina yao kupokelewa.

Wakati huo huo, Prof. Ndalichako amesema shule zikifunguliwa, wanafunzi wengine watasoma hadi tarehe 18 Desemba 2020 zitakapofungwa.

Amezitaka shule za bweni kuweka utaratibu wa wanafunzi kuanza kuripoti siku tatu kabla ya tarehe 29 Juni 2020, ili kupunguza adha ya usafiri.

Prof. Ndalichako amewataka wamiliki wa shule binafsi kuwapokea wanafunzi wasiokuwa na ada na mazingira mazuri yawekwe ya ulipaji ada huku akiwataka wazazi na walezi kutoa ushirikiano katika hilo.

“Si vizuri unamkataa mtoto wa Kitanzania kwa sababu hajalipa ada, wekeaneni utaratibu na bodi za shule ziweke mfumo mzuri wa malipo ya mhula wa kwanza na wa pili ili tusianze kugawanyika na mifalakano. Lakini kubwa zaidi, busara itumike katika hili suala la malipo ya ada,” amesema Prof. Ndalichako.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Wananchi waomba msaada ukamilishaji ujenzi wa sekondari

Spread the loveWANANCHI wa Kijiji cha Muhoji, wilayani Musoma Mkoa wa Mara,...

ElimuTangulizi

Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa utoro

Spread the loveMwalimu Maganga Japhet amesimamishwa kazi na Tume ya Utumishi wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri...

Elimu

150 wahitimu Shahada ya Udaktari HKMU

Spread the loveCHUO Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), kimeiomba serikali...

error: Content is protected !!