October 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Ndalichako ateta na ujumbe wa WB, atoa ahadi

Spread the love

 

PROFESA Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania amesema, Serikali itahakikisha fedha zinazotolewa na wadau mbalimbali wa maendeleo kwa ajili ya miradi ya sekta ya elimu zinatumika kama zilivyokusudiwa. Anaripoti Glory Massamu, TUDARCo…(endelea).

Waziri Ndalichako alisema hayo jana Jumatatu, tarehe 27 Septemba 2021 jijini Dar es Salaam, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Benki ya Dunia (WB) ukiongozwa na Makamu wake wa Rais, Dk. Hafez Ghanem.

Waziri huyo ameitaka miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia pamoja na Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) (unafadhiliwa kwa ushirikiano na FDCO, SIDA, KOICA na GPE), mradi wa kukuza na kuendeleza ujuzi (ESPJ) na Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Uchumi (HEET).

Mingine ni, Mradi wa Kuongeza Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) na Mradi wa Afrika Mashari wa Kuboresha Mafunzo ya Ufundi (EASTRIP) ambayo utekelezaji wa miradi hiyo uko katika hatua mbalimbali.

“Serikali ya Tanzania inashukuru kwa ufadhili wa miradi ya sekta ya elimu ambao umetolewa na Benki ya Dunia,” alisema Profesa Ndalichako

“Utekelezaji wa miradi hii umeleta mafanikio katika ngazi zote za elimu ikiwemo ongezeko la fursa za elimu ikiwa ni matokeo ya uboreshaji wa miundombinu na mazingira ya kufundishia na kujifunzia, upatikanaji vifaa, uboreshaji wa mbinu za ufundishaji, huduma za maji salama na safi shuleni, ongezeko la walimukupelekwa katika shule nchini na uimarishaji uthibiti ubora wa shule,” alisema Profesa Ndalichako.

Alisema utekelezaji wa miradi hiyo umewezesha ongezeko katika uandikashaji katika shule za msingi kutoka 93% mwaka 2020 hadi 95.3% mwaka 2021 wakati katika ngazi ya sekondari ongezeko ni 35% mwaka 2020 hadi kufikia 37% mwaka 2021.

Profesa Ndalichako alisema, kupitia Mradi wa SEQUIP tayari serikali imepokea takribani Dola milioni 74 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa ujenzi wa shule mpya za sekondari ambazo zinatarajiwa kuchukua wanafunzi zaidi ya 300,000.

Alisema, mradi huu pia utasaidia wanafunzi wa kike zaidi milioni 3.1 kupitia shule maalum zitakazojengwa za wasichana na vituo maalum vitakazoimarishwa kwa ajili ya kutoa elimu kwa njia mbadala kwa wanafunzi waliopata mdondoko.

Akizungumzia namna utekelezaji wa miradi hiyo ilivyoongeza ufaulu, Profesa Ndalichako amesema kumekuwa na ongezeko la ufaulu kutoka 79.4% mwaka 2019 hadi kufikia 82.7% mwaka 2020 kwa shule za msingi, wakati kwa upande wa sekondari kidato cha nne ufaulu umeongezeka kutoka 80.65% mwaka 2019 hadi 85.8 mwaka 2020.

Kwa upande wa kuendeleza ujuzi kupitia mradi wa kuendeleza ujuzi (ESPJ) amesema kumekuwa na uboreshaji na kuongeza miundombinu ya ufundishaji na kujifunzia katika vyuo 54 vya Maendeleo ya Wananchi hali ambayo iimewezesha kuongezeka kwa wanafunzi wanaojiunga na vyuo hivyo kutoka 5,520 mwaka 2019/20 hadi kufikia 15,032 mwaka 2020/21 na pia mradi umewezesha ujenzi wa vyuo 29 vya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA).

Wakati huo huo, Profesa Ndalichako alisema Serikali na Benki ya Dunia zipo katika hatua za mwisho za kukamilisha majadiliano juu yamradi mpya wa kuendeleza elimu ya msingi “BOOST Project” ambaopia utafadhiliwa na Benki ya Dunia kwa Dola za Kimarekani milioni 200.

Kwa upande wake, Makumu wa Rais wa Benki ya Dunia, Dk. Hafez Ghanem alisema, benki hiyo imeiwezesha serikali ya Tanzania kufanikisha utekelezaji wa sera ya elimu ili kuwezesha kila mtoto wa Kitanzania kupata fursa ya elimu msingi.

Aidha, aliiitaka wizara hiyo kuona jinsi ya kuimarisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika ufundishaji na ujifunzaji katika ngazi zote za elimu.

error: Content is protected !!