March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Nchemba aridhia wakimbizi kurudi kwao

Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema serikali ya Tanzania haifukuzi wakimbizi kama inavyodaiwa, anaandika Hamisi Mguta.

Mwigulu amesema hayo katika kikao cha kuweka maandalizi ya kuwarejesha wakimbizi raia wa Burundi ambao walioomba kwa ridhaa yao kurudi nchini kwao.

“Serikali ya Tanzania haifukuzi wakimbizi, tunaunga mkono hiari yao ya kuondoka, wenyewe kwa kuwa waliishinikiza serikali kwa kufanya fujo ili walirudishwe kwao na mimi kama waziri mwenye dhamana niliwaambia sitaongeza polisi kupambana na watu wanaotaka kurudi kwao,” amesema.

Amesema kuwa Tanzania inaendelea na majukumu yake yaliyobainishwa kwenye mikataba ya kimataifa ya kupokea na kutunza wakimbizi na mpaka sasa Tanzania ina Wakimbizi zaidi ya 351,400 kutoka Burundi na Kongo.

“Wakimbizi 73,000 wanatoka Kongo na 277,535 wanatoka Burundi. na 150 ni wabantu kutoka Somalia na 338 ni wa kutoka mataifa mengine,”amesema.

Aidha, ameeleza kuwa sheria za kimataifa zinaelekeza kwamba kama watu watajiandikisha kwa ridhaa yao kwamba wanataka kurudi walipotoka na wana uhakika kuwa sababu iliyowafanya wakimbie haipo tena.

error: Content is protected !!