May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Mwigulu ajipendelea kodi kwenye ‘kampuni yake’

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba

Spread the love

 

WAZIRI wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba, amegundulika kuwa na mgongano wa kimaslahi, kufuatia taarifa kuwa mke wake wa ndoa, ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya michezo ya kubahatisha. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali serikalini zinasema, mke wa Dk. Mwigulu, anayefahamika kwa jina la Neema Wilfred Ngure au Neema Mwigulu Nchemba, ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Extrabet Limited.

Fadhili Emmanuel Nkurlu, aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ambaye ni mmoja wa wanahisa wa kampuni ya mke wa Mwigulu, amethibitisha kuwa Neema ni mkurugenzi mwaanzilishi wa kampuni hiyo, iliyosajiliwa tarehe 1 Desemba 2020.

Wakati Neema anaanzisha kampuni hiyo, Mwigulu alikuwa waziri wa Katiba na Sheria. Nyaraka kutoka Wakala wa Serikali wa Leseni na Biashara (BRELA), zinaonyesha kuwa Neema anamiliki asilimia 77 ya hisa kwenye kampuni hiyo ya michezo ya kamari.

Undani wa habari hii ikiwemo mahojiano na Nkurlu, soma Gazeti la Raia Mwema, toleo la leo Ijumaa tarehe 23 Julai 2021.

error: Content is protected !!