July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Mukangara ‘akimbia’ waandishi

Fenella Mukangara Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Spread the love

FENELLA Mukangara-Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ametia doa hafla ya utoaji tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2014, zinazoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT). Amealikwa hakuja wala hakutuma mwakilishi. Anaandika Mwandishi Wetu… (endelea)

Tuzo hizo zimekabidhiwa jana na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Billal ambapo waandishi 44 walioteuliwa na majaji walichuana katika makundi 21.

Siri ya “utoro” wa Dk. Mukangara ilifichuka wakati Jaji mkuu wa jopo lililopitia kazi za waandishi hao, Chrysostom Rweyemamu alipokuwa akitoa taarifa ya mchakato mzima ulivyokwenda mbele ya mgeni rasmi.

Rweyemamu alianza kwa kuwatambua wageni waalikwa kulingana na nafasi zao za uongozi. Alimtaja Dk. Mukangara lakini alipoinua macho meza kuu, akasita kidogo na kusema “simuoni waziri Mukangara…nadhani hajafika.”

Kwa mujibu wa ratiba, Dk. Mukangara ndiye alipaswa kusema neno fupi la kumkaribisha mgeni rasmi ahutubie hadhara, badala yake kazi hiyo ikabidi ifanywe na Jaji mstaafu Thomas Mihayo-aliyepia Rais wa MCT.

Haikufahamika mara moja sababu ya kutofika kwake au mwakilishi wake, lakini pia MCT hawakutoa ufafanuzi wowote kama alikuwa ameomba udhuru au la.

Hali hiyo iliibua minong’ono ya hapa na pale ukumbini. Baadhi ya waandishi wakadai kwamba amekwepa asibanwe kuhusu Muswada wa Habari (2015), uliosomwa na Serikali kwa mara ya kwanza bungeni ukiwa umeacha maoni ya wadau. 

Akizungumza kabla ya kukabidhi tuzo kwa washindi, Dk. Bilal aliwata waandishi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na weledi hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu ili kuisaidi jamii kuepuka vurugu.

Washindi bora wa jumla kwa mwaka 2015 ni Mkinga Mkinga na Lucas Liganga wa gazeti la The Citizen huku tuzo ya mwanahabari bora wa maisha ikitwaliwa na Jenerali Twaha Ulimwengu.

Washindi hao pamoja wengine walikabidhiwa zawadi mbalimbali zikiwemo tuzo, fedha, runinga, kompyuta mpakato, simu na vyeti vya utambuzi.

error: Content is protected !!