January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Muhongo ajiuzulu, aahidi kutoa ukweli

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akizungumza na waandishi wa habari

Spread the love

WAZIRI wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ameandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kuomba kujiuzulu wadhifa wake, anaripoti Erasto Stanslaus.

Prof. Muhongo amefikia hatua hiyo baada ya kushutumiwa kuwa miongozi waliohusishwa na sakata la uchotwaji wa mabilioni ya fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo jijini Dar es Salaam, Profesa Muhongo ameamua kufikia maamuzi hayo mazito kwa lengo la kumaliza mjadala wa Escrow ili mambo mengine ya msingi ya kitaifa yafanyike.

Prof. Muhongo anasema kujiuzuru kwake kutaisaidia serikali na bunge kumaliza malumbano ya sakata hilo ambalo linazidi kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Pamoja na kujiuzuru lakini anasisitiza kuwa yeye si mwizi na hawezi kuuza utu wake kwa kupewa rushwa ili kuwakandamiza watanzania.

“Nimejiuzuru bila kushinikizwa na mtu yeyote. Mimi ndiyo nitamaliza mjadala huu wa sakata la Escrow, nchi ina mambo mengi ya kitaifa yanayotakiwa kujadiliwa lakini watu wamekazana na Escrow, nimemuandikia Rais barua rasmi ya kujiuzuru wadhifa wangu,” alisema Profesa Muhongo.

Prof. Muhongo anasema baada ya kujiuzuru anatarajia kuwaeleza watanzania ukweli wa sakata la Escrow na kujiuzuru kwake ili kuvunja majungu yanayoendelea kuitesa Tanzania na watu wake.

Mbali ya hayo Prof. Muhongo ameelezea furaha yake ya kupatikana kwa maendeleo ya haraka katika wizara yake kwa kipindi chake akisema kuwa nidhamu na uwajibikaji vilikuwa dira ya maendeleo wizarani hapo.

MwanaHALISI Online litakuletea habari zaidi hivi punde

error: Content is protected !!