October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri mkuu wa zamani wa Lesotho ashitakiwa kwa kumuua mkewe

Spread the love
WAZIRI Mkuu wa zamani wa Lesotho, Thomas Thabane amefikishwa mahakamani anakoshitakiwa kwa mauaji ya mke wake, Lipolelo Thabane, yaliyotokea mwaka 2017. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mkewe wa sasa, Maesaiah, alishitakiwa kwa uhalifu kama huo mwaka jana.

Alikuwa akiishi na Bw Thabane wakati wa mauaji hayo na wanatuhumiwa kuajiri watu waliotekeleza shambulizi hilo. Wote wawili wamekana kuhusika na tuhuma hizo.

Niliokoa maelfu ya wanawake katika ndoa kama yangu. Afungwa kifungo cha maisha mara mbili kwa kumuua mke wake kwa nyoka aina ya cobra.

Bw Thabane alijiuzulu Mei mwaka jana, kufuatia shinikizo la miezi kadhaa kutoka kwa wananchi, baada ya kutajwa kama mshukiwa muhimu kwenye mauaji hayo.

Kesi hiyo imewashangaza wengi na kusababisha misukosuko ya kisiasa katika ufalme huo mdogo usio na bahari ambao umezungukwa kabisa na Afrika Kusini.

Maesaiah Thabane aliandamana na waziri mkuu huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 82 hadi mahakamani. Alishitakiwa mwaka jana na kisha kuachiliwa kwa dhamana.

Mashitaka hayo yalisomwa katika ukumbi wa Mahakama Kuu katika mji mkuu wa Maseru, badala ya chumba cha mahakama kuu, jambo ambalo ni la kawaida.

Watu wenye silaha walimpiga risasi na kumuua Lipolelo Thabane, tarehe 14 Juni 2017 – siku mbili kabla ya Bw Thabane kuapishwa kuwa waziri mkuu.

Alipatwa na mkasa huo, wakati akirejea nyumbani.  Aliviziwa, akapigwa risasi mara kadhaa akiwa karibu na akafa kando ya barabara. Alikuwa na umri wa miaka 58.

Wakati huo, Lipolelo alikuwa katikati ya kupata talaka kutoka kwa Bw Thabane na alikuwa akiishi tofauti na mume wake, tokea mwaka 2012.

Alikuwa amehama kuanza kuishi na Maesaiah kwa muda kati ya 2012 na 2017. Walioana miezi miwili baada ya kifo cha Lipolelo.

error: Content is protected !!