
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron
WAZIRI Mkuu wa Uingereza David Cameron amesema hatawania muhula wa tatu kwa nafasi ya uwaziri mkuu endapo chama chake cha Conservative kitashinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Katika mahojiano na BBC yaliyofanyika siku ya Jumatatu, Cameron aliahidi kutumikia miaka 5 kamili kama chama chake kitaendelea kubaki madarakani baada ya uchaguzi Mei 10 mwaka huu, “nitapenda kumalizia mambo yaliyobaki kwenye sekta ya elimu na afya” alisema.
“Muda wa kuwepo madarakani ni sawa na ‘shredded wheat’ (akimaanisha aina fulani ya mikate) — mikate miwili ni barabara, lakini mitatu ni mingi sana”, Cameron alisema.
Cameron alisema kuna viongozi wenye ‘macho mapya’, Conservative kina watu wenye uwezo wanaokuja juu, huku akiwataja Theresa May Waziri wa Mambo ya Ndani, George Osborne Waziri wa Fedha na Meya wa London, Boris Johnson kuwa ni watu wanaoweza kushika nafasi hiyo.
Mahojiano haya ya Waziri Mkuu yalivuruga siasa Uingereza. David Alexander mkuu wa kitengo cha mikakati cha chama cha Labour mpinzani mkuu wa Conservative alisema Conservative wasifikirie kuwa wananchi wa Uingereza wataunga mkono Conservative wakati sio kweli.
“Cameron kufikiria muhula wa tatu hapo 2020 kabla waingereza hawajapewa nafasi ya kufanya uamuzi kwenye uchaguzi wa mwaka huu ni majigambo na kupenda makuu”, Alexander alisema.
Uingereza haina kikomo cha waziri mkuu kuwepo madarakani, ilimradi bunge la Uingereza liendelee kuwa na imani na awe kiongozi wa chama cha siasa kinachowakilisha viti vingi.
Uingereza inafanya uchaguzi kila baada ya miaka 4. Waziri Mkuu aliyekaa muda mrefu zaidi ni Margaret aliyeanza Mei 1979 mpaka Novemba 1990.
More Stories
Chadema yatangaza mchakato mrithi wa Halima Mdee
Mkurugenzi Jiji la Dar, ahamishiwa Kinondoni
Sita wadakwa kwa utakatishaji fedha Bil 4.78