August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Mkuu Uingereza: Kujitoa EU ni kazi ngumu

Theresa May, Waziri Mkuu wa Uingereza

Spread the love

 

Theresa May, Waziri Mkuu wa Uingereza ahofia azma yake ya kujitoa kwenye Jumuiya ya Nchi za Umoja wa Ulaya (EU), anaandika Wolfram Mwalongo.

Ikiwa ni miezi mitano imepita tangu kura ya maoni ipigwe na Waingereza kuamua kujiondoa kwenye umoja huo, waziri huyo ameonesha wazi wasiwasi wa kufikia azma hiyo.

May amesema nidhahiri majadiliano ya nchi yake na nyingine 27 wanachama wa umoja huo yatakuwa magumu kutokana na kwamba, hawataki nchi ziendelee kujitoa uanachama.

Ameongeza kwamba, hatua zenye utulivu zinapaswa kuchukuliwa sasa kuhusu kujitoa rasmi kwenye kwenye umoja huo.

May ameanza kuona ‘kiti cha moto’ kutekeleza azma hiyo kutokana na ugumu atakaoenda kukabiliana  nao katika mjadala utakaohusisha nchi wanachama ingawa amekiri wazi kwamba, anategemea kuendeleza uhusiano na mataifa yote 27 ambayo ni wanachama wa EU.

Tarehe 23 mwezi Juni mwaka huu, Uingereza ilipiga kura ya kujitoa kwenye umoja huo ikidai kutoona manufaa yoyote huku baadhi wakiona manufaa ndani ya Jumuiya hiyo.

Asilimia 52 ya kura ilifanikisha  kuwaondoa Waingereza kwenye umoha huo huku wengine wakiangua kilio.

David Cameroon, Waziri Mkuu Mstaafu wa taifa hilo alilazimika kuachia ngazi kutokana na kutoafiki azma hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na May aliyeunga mkono hatua hiyo.

May alipata Uwaziri Mkuu kutokanaka na msimamo wake wa kuunga mkono Waingereza walioamini kwamba, nafasi za ajira na masoko mengi ya biashara nchini humo yalitekwa na mataifa ya kigeni.

Wachambuzi wa masuala ya uchumi walikosoa uamzi huo kwa madai kwamba, huenda ingeyumbisha uchumi wa taifa hilo hususan kutokana na kupoteza baadhi ya hisa zake  EU.

Uingereza ilituma maombi ya kujiunga na umoja huo mwaka 1973 na kukubaliwa rasmi mwaka 1975 chini ya Waziri Mkuu wa wakati huo  Edward Health.

Hata hivyo, hatua hatua ya kujitoa kwa Uingereza katika umoja huo haikuanza siku za hivi karibuni, bali ilianza miaka ya 2000 kutokana na wananchi wa taifa hilo kupinga matumizi ya sarafu ya Euro.

Malalamiko ya Uingereza yalikuwa, sarafu ya Paundi ya nchi hiyo inaweza kuanguka hivyo juhudi za kujitoa zilipamba moto ili kuilinda.

error: Content is protected !!