May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Mkuu Uingereza kikaangoni

Spread the love

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson anajiandaa kubaki au kutoka ofisini baada ya kukamilika kwa matokeo ya uchunguzi wa sherehe zilizofanyika katika makazi yake na afisi yake ya Downing Street wakati nchi hiyo ilipokuwa imefungwa kwa ajili ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Nyaraka za matokeo hayo zitamsaidia kujua iwapo atafikia kikomo cha wiki kadhaa za sakata hilo ambalo limempaka matope mbele ya Waingereza au uongozi wake utafikia mwisho ghafla.

Ripoti zinaarifu kwamba Sue Gray anayeongoza uchunguzi huo, huenda akawasilisha ripoti yake kwa serikali hii leo tarehe 26 Januari, 2022.

Ofisi ya Johnson imeahidi kuchapisha matokeo ya uchunguzi huo na waziri mkuu huyo atalihutubia Bunge kuhusu matokeo hayo baada ya ripoti kuwasilishwa.

Ofisi ya Gray haikutoa tamko kwamba ni lini itatoa ripoti yake na serikali Uingereza imesema haijapokea ripoti yoyote kufikia asubuhi ya leo.

error: Content is protected !!