Wednesday , 17 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Waziri Mkuu Uingereza aponea kung’olewa
KimataifaMakala & Uchambuzi

Waziri Mkuu Uingereza aponea kung’olewa

Polisi wa Uingereza wakikabiliana na waandamanaji waliokuwa wakipinga vizuizi vya Covid-19
Spread the love

 

WAZIRI mkuu wa Uingereza, Boris Johnson aponea chupu chupu kuondoka madarakani, kufuatia kura ya kutokuwa na imani naye kushindwa kufaulu. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).

Kura ya kutokuwa na imani dhidi ya Johnson ilipigwa jana katika Bunge la Uingereza, lakini idadi kubwa ya wabunge kutoka chama chake cha Conservative, wakipiga kura ya “ndio” kuunga mkono kuondolewa kwake madarakani.

Uasi katika chama chake juu ya kashfa ya “partygate,” unaonekana kuwa pigo kwa mamlaka yake na kumwacha waziri mkuu huyo katika nafasi mbaya ya kutafuta uungwaji mkono.

Johnson ambaye alipata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa mwaka 2019, amekuwa chini ya shinikizo kubwa baada ya kuandaa sherehe ya unywaji pombe katika ofisi yake ya Downing Street na makaazi yake wakati taifa lake, lilipokuwa chini ya vizuizi vikali vya Corona.

Katika siku za hivi karibuni, Johnson alizomewa wakati wa hafla ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 70 ya uongozi wa Malkia Elizabeth, inayojulikana kama Jubilee ya Platinum.

Wabunge kadhaa wamesema kura hiyo ya kutokuwa na imani na Johnson, ambapo wabunge 211 walipiga kura ya kumuunga mkono huku wabunge 148 wakipiga kura ya kutaka kumng’atua madarakani, licha ya kushindwa, imechora taswira mbaya tofauti na ilivyotarajiwa kwa waziri mkuu ambaye alionekana kuwa na ushawishi mkubwa bungeni baada ya kupata wingi wa viti kwa zaidi ya miongo mitatu.

Hata hivyo, ni mapema mno kujua kitakachotokea baada ya kura ya leo. Waziri wa zamani David Jones, ameliambia shirika la habari la Reuters, “Boris Johnson atapata nafasi ya kupumua baada ya kura ya leo lakini pia anafaa kuelewa kipaumbele kinachofuata ni kujenga upya mshikamano wa chama.”

Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson

Lakini baadhi ya wabunge wameonyesha matumaini madogo kwa uongozi wake.

Mbunge mmoja wa chama cha kihafidhina ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema, “ni wazi kuwa matokeo ya kura hii, ni mabaya tofauti na ilivyotarajiwa na wengi. Ni mapema mno kusema kitakachotokea baada ya hapa.”

Kwa kuponea kura ya kutokuwa na imani naye, Johnson amepata nafasi ya kupumua kwa angalau miezi 12 mengine ya kujipanga.

Mtangulizi wake Theresa May, licha ya kupata kura nyingi zaidi tofauti ya Johnson wakati wa kura ya kutokuwa na imani naye mwaka 2018, alijiuzulu wadhfa wake miezi sita baadaye.

Baada ya kura hiyo bungeni, waziri mkuu amesema hana nia ya kuandaa uchaguzi wa kitaifa licha ya baadhi kupendekeza afanye hivyo ili kurejesha mamlaka yake.

Amewaambia waandishi habari kuwa matokeo ya kura hiyo ni imara na ya kuridisha, akimaanisha kwamba serikali inaweza kushughulikia mambo mengine muhimu.

Lakini licha ya ushindi wake, wabunge kadhaa wa chama cha kihafidhina wameelezea wasiwasi wao juu ya iwapo Johnson mwenye umri wa 57 amepoteza mamlaka ya kuitawala Uingereza, ambayo inakabiliwa na hatari ya kuporomoka kiuchumi na kupanda kwa bei ya chakula na mafuta.

Hata hivyo, baraza lake la mawaziri limejitetea kwa kufafanua mafanikio waliyoyapata serikalini ikiwemo utoaji haraka wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa ugonjwa wa UVIKO-19, na mwitikio mzuri wa Uingereza kwa mzozo wa Ukraine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

‘Mwanapekee’ wa Rais Samia: Atabadili nini Arusha?

Spread the loveMAPEMA wiki hii, baadhi ya viongozi walioapishwa na Rais Samia...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kipunguni waihoji serikali, ziko wapi fedha za fidia?

Spread the loveWATU wanaodai kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu,...

Habari za SiasaMakala & UchambuziTangulizi

Askofu Bagonza: Tusichonganishwe; tusichokozane na tusikufuru

Spread the loveJOTO la chaguzi linapanda kila siku hapa nchini. Upo umuhimu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

error: Content is protected !!