August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri mkuu Uingereza agoma kujiuzulu

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson ameendelea kusisitiza kuwa hatojiuzulu licha ya kuendelea kushinikizwa kufanya hivyo kutokana na kashfa mbalimbali zinazoiandama serikal yake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kashfa hizo zimesababisha baadhi ya maofisa wa serikali, Waziri wa afya, Sajid Javid na waziri fedha Rishi Sunak kujiuzulu kwa kile wanachosema hawana imani na Waziri Mkuu Boris.

Hayo yanajiri baada ya Waziri mkuu huyo kuomba radhi kwa kile alichokieleza kuwa hakufahamu kuwa mmoja wa wafanyakazi wa serikali, ambaye pia ni Waziri wa zamani, alihusika na utovu wa nidhamu wa kingono, pia nay eye binafsi kufanya sherehe na kukiuka masharti ya corona kipindi hicho.

Jana tarehe 7 Julai, 2022 Johnson amewambia wabunge kwamba ataendelea kutekeleza majukumu yake, licha ya shinikizo hilo.

Aidha, mawazi kadhaa wakiwemo wandani wake Johnson, kama vile waziri wa uchukuzi Grant Shapps, wanatarajiwa kuandaa kikao naye kumshawishi ajiuzulu.

Katika hatua nyingine Johnson amemfuta kazi mmoja wa mawaziri wake Michael Gove, huku chama chake cha Conservative kikitarajiwa kukutana wiki ijayo kuangalia upya kanuni za chama ili kuitisha kura ya kukosa imani naye, wakati ou huo waziri mweingine Simon Hart, pia amejiuzulu.

error: Content is protected !!