August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Mkuu: Ninasikitika kuacha kazi nzuri zaidi duniani

Spread the love

 

“Ninasikitika kuacha kazi nzuri zaidi duniani lakini ndiyo hali halisi”, hayo ni maneno ya Waziri Mkuu wa Uingerea, Boris Johnson ambaye leo tarehe 7 Julai, 2022 ametangaza kujiuzulu wadhifa huo na sasa mchakato wa kumpata mrithi wake utaanza mapema wiki ijayo.

Akihutubia umma mbele ya vyombo vya habari, Kiongozi huyo amesema “Ninataka mjue jinsi ninavyohuzunishwa na kuacha kazi bora zaidi duniani.

“Nimekubaliana na Sir Graham Brady, mwenyekiti wa wabunge wetu wa viti maalum, kwamba mchakato wa kumchagua kiongozi mpya uanze sasa na ratiba itatangazwa wiki ijayo,” amesema na kuongea kuwa leo ameteua Baraza la Mawaziri kuhudumu huku yeye pia akiendelea kuongoza hadi kiongozi mpya atakapochaguliwa.’

“Inatia uchungu kutoona miradi yangu ikikamilika bila usimamii wangu, hata hivyo, ni jambo la kipuuzi kubadilisha serikali – na kukataa wazo la uchaguzi mkuu katika hali kama hii,” amesema.

Aidha, Johnson ambaye amehudumu katika nafasi hiyo kwa miaka mitatu, ameshukuru umma kwa upendo mkubwa waliomuonesha.

“Zaidi ya yote, ninataka kuwashukuru ninyi, umma wa Uingereza, kwa upendeleo makubwa mliyonipa,’’ amesema.

Amesema umma utahudumiwa kuanzia sasa hadi waziri mkuu mpya atakapochukua wadhifa huo.

Waziri mkuu amemaliza hotuba yake kwa kusema kwamba hadi pale atakapopatikana mbadala wake, maslahi ya umma yatatekelezwa.

“Kuwa waziri mkuu ni elimu ya kipekee – nimesafiri kila sehemu ya Uingereza na nimekutana na watu wengi wenye asili ya Uingereza ambao pia wako tayari kushughulikia matatizo ya zamani kwa njia mpya.

“Hata kama mambo yanaweza wakati mwingine kuonekana kuwa na giza nene, mustakabali wetu kwa pamoja ni jambo muhimu zaidi,’’ Johnson amesema huku akipigiwa makofi anapoondoka.

error: Content is protected !!