ELIZABETH Sumaye, aliyekuwa mama mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye amefariki dunia jana tarehe 7 Novemba 2018 nyumbani kwake kijijini Endasaki wilayani Hanang mkoa wa Manyara. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).
Taarifa zinaeleza kuwa, marehemu Elizabeth amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo na mapafu.
Kufuatia msiba huo, chama cha Chadema kupitia Katibu Mkuu wake, Dk. Vincent Mashinji kimetoa salamu za pole na rambi rambi kwa familia ya Sumaye.
“Chama kitaendelea kushirikiana na familia ya Mzee Sumaye kutoa taarifa kuhusu msiba huo ambao shughuli zake, ikiwemo mazishi zitafanyika kijijini Endasaki,” inaeleza taarifa ya Chadema iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na MawasilianoTumaini Makene.
Leave a comment