June 24, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Mkuu kuhamia Dodoma, Septemba mwaka huu

Spread the love

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amemwagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na walemavu Jenister Muhagama na makatibu wakuu kuhakikisha wanamaliza nyumba yake ifikapo mwezi wa tisa mwaka huu ili aweze kuhamia, anaandika Dany Tibason.

Mbali na hilo  amewataka mawaziri pamoja na Manaibu Waziri kuhakikisha wanahamia Dodoma mara moja kwa kuwa wana nyumba za kutosha za kuishi na ofisi ndogo.

Ametoa kauli hiyo jana na Maajaliwa baada ya kupewa nafasi na rais John Magufuli wakati alipopewa nafasi ya kuwasalimia wananchi wa mji wa Dodoma wakati wa maadhimisho ya siku ya Mashujaa.

Majaliwa amesema yeye kama waziri mkuu ndiye wa kwanza kupewa maagizo na mkuu wake ambaye ni Rias ili aweze kuhamia Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha mawazo na nia ya Mhasisi wa taifa la Tanzania hayati baba wa Taifa Julias Kambarage Nyerere ya kuhamia Dodoma.

Majariwa amesema ana uhakika iwapo nyumba yake itakuwa imekamilika nay eye kuhamia Dodoma ni wazi kuwa kila waziri na viongozi wengine watahamia Dodoma.

Kutokana na kusudio la serikali kuhamia Dodoma amewataka watanzania pamoja na wakazi wa mji wa Dodoma kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kuboresha shughuli zao.

“Nataka kuwahakikishia wananchi wa mkoa wa Dodoma kitendo cha serikali kuhamia Dodoma kitaongeza ufanisi wa kazi zenu na ninawashauri kuwekeza kwa kuboresha huduma zenu, kuongeza ujenzi wa mahoteli makubwa na mazuri pamoja na nyumba za kulala wageni.

“Mji huu utakuwa na ugeni mkubwa hivyo rai yangu kwenu ni kuhakikisha mnaboresha kila huduma na kuwa katika kiwango bora ili wageni wanaokuja hapa wapate huduma nzuri nay a uhakika” ameeleza Kassimu.

Naye rais wa Tanzania John Magufuli, amesema kamwe hawezi kudharau mawazo ya Mwalimu nyerere ambayo yalikuwa na lengo la Dodoma kuwa makao makuu.

“Mimi siwezi kukubali kuona Dodoma haiwi makao makuu wakati bunge lenye wabunge zaidi ya 300 wanakuja Dodoma na kukaa hapa siku zote, chama change ninachokiongoza kipo hapa makao makuu, hivyo kwa miaka yangu mnne na miezi mine iliyobaki nitahakikisha Dodoma inakuwa makao makuu ya nchi.

“Ninamuomba Mungu ili niweze kufikia hatua hiyo ambayo ya kuufanya mkoa wa Dodoma kuwa makao makuu na mimi najua wazi kuwa nikihamia Dodoma watu wote watanifuata”amesema.

Katika hatua nyingine Magufuli amesema anamuomba Mungu akimaliza kipindi chake ama akitangulia mbele ya haki aihache Tanzania katika hali salama ya utulivu wa amani.

Amesema Tanzania imekuwa ikisifika ndani ya nchi na nje ya nchi kuwa ni nchi ya amani hivyo asiwepo mtu hata mmoja ambaye atadhutubu kuchezea amani ya nchi.

“Natamani kuacha nchi ya Amani,katika kipindi ambacho nitamaliza muda wangu hata nikiwa nimetangulia mbele ya haki, nataka kuliona taifa lenye watu wenye amani na utulivu na siyo nchi ambayo haina Amani” amesema Rais Magufuli.

Mwinyi azungumza,

Naye rais wa awamu ya pili, All Hasani Mwinyi amesema kitendo cha serikali ya awamu ya tano kuona umuhimu wa Dodoma kuufanya mkoa wa Dodoma kuwa makao makuu ni wazo la la msingi na la kumuhenzi baba wa taifa.

Mbali na hilo amesema serikali ikihamia Dodoma ni wazi kuwa lengo hilo la miaka mingi litakuwa limetimia na serikali itakuwa imetekeleza mpango ambao wa Dodoma kuwa makao makuu.

Maoni ya wananchi,

Baada ya viongozi hao kutoa hotuba zao wananchi nao wameitaka serikali kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya uhakika ili kuepusha usumbufu ambao unaweza kujitokeza.

Mmoja wa wananchi aliyezungumza na Tanzania daima John Mahelela,alisema serikali inatakiwa kuhakikisha inaweka miundombinu abayo itaondoa usumbufu ambao unaonekana kulikumba jiji la Dar es Salaam.

error: Content is protected !!