Monday , 22 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri Mkuu kufungua maonyesho ya Azaki
Habari za Siasa

Waziri Mkuu kufungua maonyesho ya Azaki

Spread the love

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, anatarajiwa kufungua maonyesho ya wiki la Asasi za kiraia  nchini leo ambapo zaidi ya mashirika yasiyo ya kiserikali 400 yatashiriki, kuanzia Oktoba 22 hadi 26 mwaka huu jijini Dodoma. Anaripoti Danny Tibason, Dodoma … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jiji hapa Mkurugenzi mtendaji wa The Foundation For Civil Society, Francis Kiwanga alisema kuwa lengo la maonyesho hayo ni kuonyesha mafanikio ya shirika hilo katika maendeleo ya Taifa.

Alisema kuwa The Foundation For Civil Society imepata mafanikio mengi hapa nchini katika maeneo mbalimbali ya kimaendeleo huku akisema kuwa asasi nyingi zimejitahidi kufanya vizuri na kutimiza malengo ya kusaidia jamii.

Kiwanga alisema kuwa katika maonyesho hayo wanatarajia kuonyesha mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika kuziwesha jamii katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo masuala ya utawala bora na uwajibikaji.

Alisema kuwa mpaka hivi sasa wanafanya kazi na Asasi zaidi ya 150 nchini ambazo wanaziwezesha katika kuzipatia ruzuku.

Aidha alisema kuwa katika maonyesho hayo pia wataangalia namna gani wanaweza kushiriki katika kuchangia katika mkakati wa Tanzania ya viwanda ifikapo 2025.

“Pia maonyesho haya tutayatumia kuwa karibu na viongozi wa serikali, bunge, taasisi binafsi pamoja na wananchi kwa ujumla ili waweze kufahamu nini tunafanya na kuondoa dhana iliyopo ya kuwa sisi tupo kwajili ya manifaa yetu,” alisema.

Alifafanua kuwa hivi sasa wameweka mikakati ya kuhakikisha kila fedha inayotolewa kama ruzuku kwa asasi mbalimbali zinatumika ipasavyo.

“Sasa hivi tumeweka mikakati kila fedha ianyotoka kama ruzuku lazima itumike vizuri na mashirika mengi yameweza kufanya vizuri kwa asilimia kubwa lengo letu sio kujinufaisha sisi,” alisema.

Mbali na mambo mengine Kiwanga alisema kuwa asasi zinalenga kuhakikisha wanakuwa karibu na serikali katika kufanya maendeleo na kutoa ushauri kwa serikali kwa nia ya kuboressha sera mbalimbali za kimaendeleo pale inapobidi.

“Asasi za kiraia siyo adui wa serikali kazi kubwa ni kupeleka mkono pale ambapo serikali haijafika na jambo kubwa zaidi ni kuchochea maendeleo kwa jamii nzima kwa na makundi mbalimbali ambayo yanatakiwa kufikiwa kama vile makundi ya watu maalum na wenye mahitaji maalumu ili waweze kutambua haki zao na kupata haki zao,” alisema Kiwanga.

Pamoja na maonesho hayo kutakuwepo na maonesho mbalimbali pamoja na utoaji wa elimu kwa Umma hususani uelimishaji kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda pamoja na utoaji huduma ya msaada wa kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari Racheli Chagonja alisema kuwa kutakuwepo utoaji wa elimu juu ya matumizi ya mafuta,madini na gesi na kuhamasisha wananchi kuweza kutumia rasilimali walizomazo kwa faida ya kimaendeleo na kuona umuhimu wa kuwa na Tanzania ya viwanda kama kauli mbiu ya serikali inavyoeleza.

Alisema kuwa elimu inayotolewa kwa jamii sambamba na ushauri wa kisheria ni huduma ambayo inatolewa bure bila kutoza fedha ya aina yoyote ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha wananchi kujua fursa ambazo wanatakiwa kuzitumia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

Habari za Siasa

Makamba ataja maeneo ya kuboresha mambo ya nje

Spread the love  WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika...

error: Content is protected !!