Saturday , 13 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri Mkuu awaombea ajira vijana kwa waandisi
Habari za Siasa

Waziri Mkuu awaombea ajira vijana kwa waandisi

Spread the love

WAZIRI Mkuu Kasim Majaliwa amewataka waandisi wanaosimamia majengo kuhakikisha wanatoa ajira kwa vijana ili waweze kunufaika na mradi wa ujenzi unaoendelea  mji wa serikali uliopo Mtumba jijini Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Majaliwa ametoa agizo hilo alipokuwa akifanya ziara ya kutembelea majengo ya wizara yanayojengwa mji wa serikali yanaoendelea kujengwa katika eneo hilo.

Aidha, aliwataka mafundi wanaojenga kwenye majengo hayo kuwa waaminifu na wazalendo kwa kazi wanazo zifanya, ili kuunga mkono juu za Rais wa Dk. John Magufuli ambaye anayehimiza ufanyaji wa kazi kwa bidii.

Pamoja na hayo amewataka wanaosimamia majengo hayo kuhakikisha yanakamilika kwa muda uliowekwa kwa kuwa serikali tayari imeshatoa fedha kwa ajili ya ujenzi huo wa majengo ya wizara.

“Nyie mainjinia na wasimamizi wengine wa majengo haya ya wizara muhakikishe hadi tarehe  31 Januari mwaka huu, yawe yamekamilika yote kama tulivyo kubaliana,” alisema.

Kwa upande wake Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akizungumza kwenye eneo la ujenzi la wizara hiyo alimwakikishia kwa kusema kuwa hadi kufikia tarehe 31 Januari litakuwa limekamilika

Alisema kutokana na agizo tuliloagizwa ninakuhakikishia tutakamilisha kwa wakati kwa kuwa ujenzi unafanyika kwa haraka na makini kutokana na ushirikiano uliopo kati ya wafanyakazi wa kampuni iliyopewa ukadarasi ya Suma pamoja na watumishi.

Hata hivyo akizungumza kwenye ziara hiyo alisema kuwa jumla ya miti  800 tayari imeandaliwa pia kwa ajili ya kupanda kwenye eneo hilo ikiwemo ya matunda na ya kawaida ili kutunza mazingira .

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Nchimbi aanika ugonjwa wa CCM

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emanuel Nchimbi,...

Habari za Siasa

Chadema yapuliza kipyenga uchaguzi viongozi kanda

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza maandalizi ya uchaguzi...

Habari za Siasa

CCM :Hatutaki ushindi wa makandokando uchaguzi Serikali za mitaa

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakihitaji ushindi wa makandokando katika...

Habari za Siasa

Makala: Puuzeni wanasiasa wanaojigamba wanaweza kubadili maamuzi ya mahakama

Spread the loveKATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...

error: Content is protected !!