Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Waziri Mkuu atawazwa tena katikati ya giza nene
Kimataifa

Waziri Mkuu atawazwa tena katikati ya giza nene

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed
Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed ameapishwa kutumikia muhula wa pili katika nafasi hiyo huku taifa lake likikumbwa na mzozo wa kidiplomasia juu ya vita vya Tigray. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi huo ambao ulisusiwa na vyama vya upinzani nchini humo, Abiy ameapishwa jana tarehe 4 Oktoba, 2021 mbele ya Rais wa nchi hiyo, Sahle-Work Zewde, katika makao makuu ya Bunge la nchi hiyo.

Baada ya uapisho huo Abiy anatarajiwa kutangaza serikali yake ndani ya wiki hiyo itakayohudumu kwa kipindi cha miaka mitano.

Aidha, baada ya sherehe ndogo katika makao makuu ya Bunge, waziri mkuu mpya alielekea katika eneo la Meskel, katikati ya mji mkuu wa Ethiopia ambapo sherehe rasmi ya kutawazwa ilifanyika na Abiy kulihutubia taifa.

Kwa hafla hiyo, wakuu saba wa nchi za Afrika wamehudhuria sherehe hizo ambao ni pamoja na marais wa Uganda, Kenya, Senegal na Nigeria.

Hayo yanajiri wakati Serikali hiyo ya Ethiopia iliwafukuza maofisa saba wa UN siku moja kabla ya uapisho huo na sasa inakabiliwa na vikwazo zaidi vya Marekani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!