December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Mkuu astukia ufisadi Dodoma

Spread the love

KASSIM Majaliwa, Waziri Mkuu amestukia ufisadi wa Sh. 1.2 bilioni  katika sekta ya kilimo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akiwa kwenye ziara  yake wilayani Chamwino, Dodoma Majaliwa amepokea taarifa ya ubadhirifu wa fedha hizo zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya mradi wa umwagiliaji ambazo matumizi yake hayajulikani

Akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Mpwayungu, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mpwayungu amemuagiza Dk. Bilinith Mahenge, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amuagize Ofisa Kilimo wa Mkoa huo Bernad Abraham kwenda kwenye mradi huo kwa ajili ya ukaguzi ili kubaini wezi wa pesa hizo.

Wakati huo huo  Waziri Mkuu alivunja kamati ya kusimamia huduma maji ya kijiji cha Mpwayungu na alimuagiza Mhandisi wa Maji wa wilaya ya Chamwino, Godfrey Mbabaye aunde kamati mpya.

Waziri Mkuu alichukua hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na utendaji wa kamati hiyo ambayo ilishindwa kutekeleza majukumu yake ikiwemo ujenzi wa vituo vya kuchotea maji licha ya kukusanya Sh. 20 milioni kwa mwezi, mradi huo unavituo vinne tu.

error: Content is protected !!