January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Mkuu apiga mkwara watumishi

Spread the love

WAZIRU Mkuu wa Tanzania, Majaliwa Kasim amewataka watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) kufanya kazi kwa weledi ili kushughulikia matatizo yote yaliyotajwa katika hotuba ya Rais John Magufuli wakati akizindua Bunge la 11. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Waziri Kasim amesema hayo leo jijini Dar es Salaam katika ziara yake kwenye Ofisi za TAMISEMI kwa lengo la kuwakumbusha watendaji hao kuzingatia hotuba ya Rais Magufuli.

Alifika katika ofisi hizo mapema mchana na kufanya kikao cha faragha na watendaji wa ofisi hiyo kilichochukua takriban dakika 45. Hata hivyo, alipotoka hakuwa tayari kuzungumza na waandishi wa habari kwa wakati huo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi hizo, Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Jumanne Abdallah amesema kuwa katika ziara hiyo Waziri Kasim amewataka watendaji kufanya kazi kwa bidii na matunda yake yaonekane.

Amesema watumishi hao wanapaswa kuwa na nakala ya hotuba ya Dk. Magufuli ili kujua mwelekeo thabiti wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Abdallah amesema pamoja na serikali kujipanga kusaidia vijiji kimaendeleo pia uongozi wa vijiji husika unatakiwa kujiwekea mikakati ya kimaendeleo ili kusaidia serikali katika kutoa huduma hizo.

Amesema kuwa, kwa uongozi wa mwaka huu jinsi ulivyojipanga, watendaji wa TAMISEMI wanapaswa kufanya kazi kwa juhudu na kuwa mtu yeyote atakayelegalega katika kazi, hatavumiliwa.

Kuhusu mgogoro unaoendelea wa bomoabomoa, Abdallah amesema zoezi hilo linafanyika kuhakikisha wanarudisha haki na kuwajibisha wanaotumia kigezo cha kuwa na fedha kujenga katika maeneo ambayo si sahihi.

error: Content is protected !!