April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Mkuu aongoza watanzania mazishi ya watu waliofariki ajali ya moto

Spread the love

KASSIM Majaliwa Waziri Mkuu Tanzania ameongoza maelfu ya watanzania mazishi ya watu zaidi ya 60 waliofariki kwenye mlipuko wa  lori la mafuta  baada ya kupinduka jana mtaa wa Itigi Msamvu mkoani Morogoro, Anaripoti Hamisi Mguta, Dodoma … (endelea).

Leo tarehe 11 Waziri Mkuu amefika Morogoro kwa ajili ya kuungana na wafiwa pamoja na watanzania kwenye kuaga miili ya watu waliofariki kwenye ajali hiyo ambapo watazikwa eneo la Kola.

“Tunatamani hawa ndugu zetu kuwazika kwenye kando ya barabara (Msamvu)  na kuweka mnara katika eneo hilo lakini ufinyu wa eneo hilo hatuna budi kwenda kuwazika eneo la Kola” amesema Majaliwa

Wakati huo huo ameeleza namna Rais John Magufuli alivyowapokea majeruhi wa tukio hilo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na kuwapa pole .

Amesema kuwa Rais Magufuli ameongea na majeruhi mmoja mmoja kwa wale wenye kuweza kuzungumza na pia ameridhishwa  na mna Muhimbili wanavyotoa huuduma kwa majeruhi.

Ameeleza kuwa waliofariki hadi sasa wamefikia idadi ya watu 72  na  majeruhi wapo 59 , waliokuwepo Hospitali ya Rufaa ya Morogoro  majeruhi 16 kule Muhimbili wapo 43.

Amewashukuru wananchi na majeshi mbalimbali likiwemo jeshi la Wananchi JWTZ, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto, na majeshi mengine nchini.

error: Content is protected !!